📌 Lengo ni kuchochea Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
📌 Asema matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia ni nafuu zaidi ukilinganisha na mkaa; Wananchi wahamasike
📌 Amtaja Rais Samia mafanikio Sekta ya Nishati
📌 Awapongeza TANESCO kutekeleza maoni ya Rais Samia kwa vitendo
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Imeelezwa kuwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kitaifa inayolenga kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi na salama ya kupikia ikiwemo nishati ya umeme.
Aidha, takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Watanzania wanaotumia nishati ya umeme kwa ajili ya kupikia ni asilimia 4.2 tu huku ikitajwa kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watanzania waliopo.
Akizungumza leo Agosti 14, 2025 jijini Dodoma wakati akizindua Mpango wa Ugawaji Majiko ya Kupikia kwa Umeme kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kutokana na historia ya siku za nyuma Watanzania walidhani kuwa kupika kwa umeme ni ghali zaidi tatizo ambalo lilisababishwa na masuala mengi ikiwemo elimu kuhusu unafuu wa gharama kwa matumizi ya umeme.
“Utafiti wa TANESCO unaonesha kuwa kupikia kwa nishati ya umeme, hasa kwa kutumia majiko janja yenye ufanisi ni nafuu zaidi kuliko wanavyofikiria wengi miongoni mwetu katika jamii tunazoishi. Utafiti huo unaonesha kuwa, majiko janja ya umeme yanaweza kutumia chini ya uniti moja (1) ya umeme ambayo ni sawa na chini ya shilingi za Kitanzania 352 kuandaa mlo mmoja,” amesema Dkt. Biteko.
Amefafanua kuwa matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia ni nafuu kuliko nishati nyingine hivyo Watanzania hawana haja ya kuogopa kutumia umeme. Aidha, hatua ya Ugawaji Majiko ya Kupikia kwa Umeme kwa Wafanyakazi TANESCO itakuwa hatua muhimu katika mabadiliko kwa kuwa wafanyakazi hao wa TANESCO watakuwa mabalozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan majiko ya umeme katika jamii.
“ Kupitia mpango huu, nimejulishwa kuwa TANESCO, kwa kushirikianana Taasisi ya Modern Energy Cooking Services (MECS) chini ya Serikali ya Uingereza imeweza kununua zaidi ya majiko 11,000. Majiko haya yatawafikia wafanyakazi wote waTANESCO kwa mpango wa mfuko wa mzunguko (revolving fund). Pia zimewekwa mbinu bunifu za ugharamiaji ambazo ni rafiki kwa kila mtumiaji,”amesisitiza Dkt. Biteko.
Amewapongeza wafanyakazi wa TANESCO kuwa kufanya kazi kubwa ya kuwahudumia Watanzania kwa kuboresha utoaji wa huduma ya umeme nchini na kuwaasa kuwa wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao sambamba na kuwa mabalozi wa mabadiliko chanya kwa jamii.
Kuhusu programu hiyo ya Ugawaji wa Majiko ya Kupikia kwa Umeme amesema hapo baadaye itahusisha wateja wa TANESCO wanaojiunga na huduma ya umeme.
“ Wateja hao watapatiwa majiko na watalipa kidogo kidogo kupitia manunuzi ya umeme (On bill financing) ilikuleta manufaa zaidi kwa jamii nzima ya Tanzania. Nawaomba TANESCO kuharakisha jambo hili iliwananchi waweze kunufaikana program hii muhimu,” ameeleza Dkt. Biteko.
Aidha, ametoa wito kwa Taasisi za Umma na Binafsi kujifunza kutoka TANESCO na kaungalia namna ambavyo watumishi wao wanaweza kunufaika na programu hiyo na kuchochoea matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kutumia umeme.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa ajenda wa nishati safi ya kupikia na kuelekeza wananchi wahamasishwe katika matumizi wa nishati safi ya kupikia.
Amebainisha kuwa hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana katika nishati ya umeme na mafuta bila kumtaja Rais Samia ambaye ametoa msukumo mkubwa katika seka hiyo si tu nchini Tanzania bali Afrika na duniani kote.
Aidha, amesema kuhusu hali ya umeme nchini, takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia Julai 2025, Tanzania ilikuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 2,720. Ambapo mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa yamefikia megawati 1,921 pekee.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga kwa upande wake, amesema kuwa, tukio la ugawaji wa majiko ya umeme kwa bei ya ruzuku kwa Wafanyakazi wa TANESCO ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Nishagi Safi ya Kupikia ambayo kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema zoezi hilo la ugawaji majiko hayo ya umeme ni kielelezo cha kuwa, Wizara ya Nishati na Taasisi zake zinaibeba Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo na pia inawafanya wafanyakazi kuwa vinara na mabalozi wa nishati safi ya kupikia.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amemshukuru Rais Samia kwa kuimarisha miradi ya nishati katika Mkoa husika kwani katika kipindi cha miaka minne ametoa shilingi bilioni 214.3 ambazo zimekamilisha miradi ya umeme vijijini na kupekeka umeme kwenye miradi mbalimbali ikiwemo umwagiliaji, afya na maji.
Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema katika Mkoa wa Dodoma majiko ya gesi takriban 10,000 yamefikia wananchi, pia miradi ya umeme jua na upepo imefikia miradi mbalimbali ikiwemo ya umwagiliaji, na taasisi mbalimbali zinatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama pamoja na Shule mbalimbali.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange alisema kuwa, tukio la ugawaji wa majiko ya umeme kwa TANESCO ni muhimu kwani ni sehemu ya mpango mkakati wa kuitikia wito wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha kuwa ifikapo 2034 asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.
Amesema majiko yatakayosambazwa ni 11,000 na yatafikia watumishi wote wa TANESCO, na hivyo ametoa wito kwa wafanyakazi kutumia majiko hayo na kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nisahati safi ya iupilia..
Mpango huo wa ugawaji majiko ya umeme amesema.kuwa, unahusisha utoaji wa elimu, usambazaji majiko na pia wananchi kukopeshwa majiko ya umeme ambapo baadaye wataweza kulipa jinsi wanavyolipia umeme lengo likiwa ni kuongeza watu wanaotumia umeme kupikia na hivyo shirika kuongeza mapato.
Mwakilishi wa mradi wa MECS uliopo chini ya Serikali ya Uingereza, ambao ndio umetoa majiko hayo ya umeme kwa wafanyakazi wa TANESCO kwa bei ya ruzuku, Charles Barnabas amesema majiko hayo yanatumia umeme kidogo.
Amesema pia wana kampeni ya kitaifa ya Pika smart ambayo wanafanya na Tanesco ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko ya umeme.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...