
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera akisaini Kitabu cha Wageni kwenye Banda la Tume ya Ushindani (FCC) katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nanenane- Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma (FCC) Bi. Roberta Feruzi katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya Nanenane - Dodoma.
....
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Dkt. Suleiman Serera, akipata elimu juu ya kazi na majukumu ya Tume ya Ushindani (FCC) katika Maonesho ya Nanenane hususan elimu ya Alama za Bidhaa, Udhibiti wa Bidhaa Bandia, Ushindani kwenye Soko na kumsaidia mkulima, mfugaji, mvuvi na mfanyabiashara ili aweze kupata tija katika shughuli za uzalishaji kupitia sekta hizo kwa kuzilinda nembo za bidhaa zao.
Dkt. Serera amepata elimu hiyo alipotembelea Banda la FCC wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi 2025 "Nanenane" yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Kaulimbiu ya Maonesho haya ni; "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...