Halmshauri ya Jiji la Dar es salaam imeibuka mshindi wa kwanza kwa Halmashauri za mkoa huo unaojumuisha halmashauri tano huku ikichukua nafasi ya tatu katika ushindi wa jumla wa Maonesho ya Nanenane mkoani Morogogoro.
Halmashauri ya Jiji imekuwa kinara ikiongoza katika halmashauri tano za mkoa wa Dar es salaam huku ikishika nafasi ya tatu katika matokeo ya jumla yaliyoshirikisha halmashauri zote na taasisi zilizoshiriki zinazounda kanda ya kati.
Maonesho hayo ambayo yamegawanywa kikanda ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo miongoni mwa halmashauri zilizopo katika kanda hii ya Mashariki ikijumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Tanga.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Elihuruma Mabelya amesema ushindi huo umetokana na ushirikiano uliopo kati ya watumishi na Menejimenti ya Halmashauri hii.
Aidha amesema ushindi huo utaongeza chachu ya kufanya kazi na kuwaletea wananchi maendeleo.
"Ninawapongeza sana kwa ushindi huu na hii imeonesha namna gani jinsi tulivyo na mshikamano katika utendaji kazi wetu, tuendelee kuwatumikia wananchi ili tumsaidie Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.'Alisema
Maonesho hayo ya wakulima maarufu kama Nanenane yaliyoanaza rasmi Agosti 1,2025 yamefikia tamati leo hii huku Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian akiyafunga Maonesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...