Na Mwandishi Maalumu

RAIS Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika (AU-AIP Water Investment Summit) unaoendelea jijini Cape Town, Afrika Kusini.

Dkt. Kikwete amehudhuria mkutano huo kwa nafasi yake ya Mwenyekiti Mwenza Msaidizi (Alternate Co-Chair) wa Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (The High Level Panel on the Africa Water Investment Programme – AIP).

Mwaka huu, Afrika Kusini ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 20 (G20). Viongozi wa Afrika wanaokutana Cape Town wanataka Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika iwe miongoni mwa ajenda kuu katika Mkutano ujao wa G20, uliopangwa kufanyika Novemba 2025 jijini Cape Town.

Mkutano huu umeitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini na Jopo la Ngazi ya Juu la AIP.

Jopo hilo linaongozwa na Wenyeviti Wenza Watatu – Rais wa Namibia, Rais wa Senegal, na Waziri Mkuu wa Uholanzi. Wajumbe wengine ni Marais wa Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Gambia, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na Mfalme wa Morocco. Dkt. Kikwete, akiwa Mwenyekiti Mwenza Msaidizi, anasaidia Wenyeviti Wenza katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkutano ulifunguliwa na Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa G20 kwa mwaka 2025. Washiriki wengine wakuu ni pamoja na Mfalme Mswati wa III wa Eswatini, Mhe. Duma Boko – Rais wa Botswana, pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali, mashirika, na wadau wa maji kutoka kote barani Afrika.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kikwete ameteuliwa kuwa mmoja wa viongozi wakuu watano wa Baraza la Uwezeshaji wa Uenyekiti wa Afrika Kusini wa G20 mwaka huu 2025, akishughulikia masuala ya maji kama Mwenyekiti Mwenza Msaidizi.

Wengine ni Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Co-Chair), Waziri Mkuu Mia Mottley wa Barbados (Co-Chair), Bw. Bill Gates – Mwenyekiti wa Mfuko wa Gates (Co-Chair), na Mheshimiwa Amina J. Mohammed – Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (Alternate Co-Chair).

 


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Mfalme Mswati III wa Eswatini katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa (kulia) na Rais wa Botswana Mhe. Duma Boko kabla ya kuanza Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na viongozi wengine katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe.James G. Bwana katika Mkutano wa Kwanza wa Uwekezaji wa Maji Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, ulioitishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Afrika Kusini pamoja na Jopo la Ngazi ya Juu la Programu ya Uwekezaji wa Maji Afrika (Africa Water Investment Programme – AIP).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...