Na Mary Margwe, Simanjiro.

Shirika lisilo la Kiserikali la ECLAT Foundation Kwa kushirikiana na Upendo Association ya Ujerumani wamejenga Shule Mpya ya Msingi ya Ole Mbole iliyojengwa Kwa gharama ya sh.mil.169.2  katika Kijiji na Kata ya Komolo, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na kukabidhi Serikali Kwa lengo kuisaidia jamii kuondokana na adha ya kupunguza msongamano wa wingi wa wanafunzi kutoka shule mama Komolo,ambapo pia kuondoka adha ya kutembea umbali mrefu 

Akikabidhi Shule hiyo Kwa Serikali Mwenyekiti wa ECLAT Foundation na CCM Mkoa wa Manyara, Peter Toima, ndiye aliyeongoza hafla ya makabidhiano hayo na kukabidhi shule hiyo kwa Serikali ya Wilaya ya Simanjiro chini ya Afisa Elimu Msingi Mwl. Marco Masala, huku mamia ya wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo.

Toima amesema Shule hiyo imegharimu shilingi Milioni 169.2, ikiwa na madarasa mawili, ofisi ya walimu, nyumba moja ya mwalimu, matundu ya vyoo 32 pamoja na madawati na meza za wanafunzi.

" Leo hii sisi Viongozi wa Shirika lisilo la Kiserikali la  ECLAT Foundation  unaikabidhi Serikali Shule mpya ya msingi ya Ole Mbole ikiwa na madarasa mawili, ofisi ya walimu, nyumba moja ya mwalimu, matundu ya vyoo 32 pamoja na madawati na meza za wanafunzi , vyote vikiwa na gharama ya sh.mil.169.2, watoto someni Sasa kama ni mazingira mazuri Sasa mmeyapata, hivyo tunawaombe Mungu kama Eclat someni Kpkwa bidii" amesema Toima.

Awali Meneja wa miradi ya Eclat Foundation Bakiri Angalia amesema Shule hiyo ilianzishwa kama shule Shikizi ikiwa na  lengo la kupunguza msongamano wa wingi wa wanafunzi kutoka katika shule mama Komolo.

" Wingi wa wanafunzi katika shule ya Msingi Komolo, ndio iliyopelekea kuwepo kwa shule Shikizi ya Olembole, ambapo Sasa wanafunzi wanasoma vizuri na miundombinu yake ni mizuri kabisa, ambapo tumejenga shule Ina  madarasa mawili, ofisi ya walimu, nyumba moja ya mwalimu, matundu ya vyoo 32 pamoja na madawati 92 na meza 4, Viti 8  vyote vikiwa na gharama ya sh.mil.169.2 " amesema Angalia.

Aidha Angalia amesema Shule hiyo ina miundombinu ya Barabara, maji ambapo  matundu 32 ya vyoo na tayari vyote vimekamilika, angapo Ina wanafunzi wa awali 120.

Katika hafla hiyo, wananchi wa Komolo walimshukuru Toima na kumzawadia ndama dume wa ng’ombe kama ishara ya kutambua mchango wake katika kufanikisha mradi huo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Komolo, Ndikoya Siara, alisema awali watoto walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita nane kufuata shule nyingine na kubanana madarasani.

“Shule hii imetupunguzia kero kubwa, tunaomba kuongezewa madarasa zaidi kwa sababu mahitaji bado ni makubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Msingi wa Wilaya hiyo Marco Masala, akipokea Kwa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya  Gracian Makota alisema ECLAT ni mfano wa a kuigwa ni mashirikamqchache  yanayoweza kuleta mwamko wa elimu katika jamii za kifugaji ambazo awali zilikuwa zikikabiliwa na changamoto ya kutowapeleka watoto shule, lakini Kwa Sasa kupitia Eclat watoto za jamii zote zinaenda shule.

Naye Mwenyekiti wa Upendo Association, Fred Heimbach, alisema furaha yao kubwa ni kuona watoto wa jamii za kifugaji wakipata elimu badala ya kuishia kuchunga mifugo.

Akizungumza baada ya kukabidhi shule hiyo, Toima aliwashukuru wafadhili na kuahidi kuendelea kutafuta rasilimali zaidi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

“Ni wajibu wa wazazi sasa kupeleka watoto shule na kuachana na mila zilizopitwa na wakati zinazokwamisha elimu ya watoto,” alisema.

Kwa kukamilika kwa ujenzi huo, Kijiji cha Komolo sasa kitakuwa na shule mbili za msingi – Komolo na Ole Mbole  baada ya kusajiliwa rasmi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...