Kilimo nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kimekua ni kitovu cha maendeleo ya Uchumi nakutoa fursa za ajira. Programu ya Shamba ni Mali ipo kwa ajili ya kupunguza changamoto zinazowakumba wakulima wadogo na wakubwa nchini. Wakulima hawaitaji tena kutegemea mvua na kubaini jinsi gani kiwango cha mafanikio ya mavuno yao yatakavyokuwa.
Programu hii ipo kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa kilimo na kulenga kuboresha maisha ya maelfu ya wakulima ndani ya Tanzania. Mpango huu umeundwa kuimarisha mbinu za kilimo, kuongeza uzalishaji, na kuhakikisha maendeleo endelevu kwa watu walioko mstari wa mbele wa sekta ya kilimo pamoja na wadau.
Shamba ni Mali ni mpango kamili ulioundwa kushughulikia vikwazo vinavyokumba maendeleo ya kilimo kwa wakulima wote wa Tanzania. Sio wakulima wakubwa tu bali unaojumuisha kila mkulima mdogo au yule anayenza kulima mtama, shayiri na mahindi. Kwa kila uzalishaji wa mkulima, kuna uhakika wa soko, kwani kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) inakubali kununua mazao yao, jambo linalosababisha mapato thabiti. Zaidi ya hayo, SBL hainunui tu mazao, bali pia inatoa mbegu bora zenye uzalishaji wa juu pamoja na mafunzo ya kina juu ya mbinu bora za kilimo kwa kilimo endelevu.
Wanawake, vijana, na makundi yasiyo na sauti yamezingatiwa katika mpango huu kwa kutoa fursa kwa kila mmoja kujiunga na kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani. Mpango huu umebuniwa kuleta mabadiliko kwa wakulima zaidi ya 4000 hadi kufikia mwaka 2030, huku ukibadilisha kilimo kutoka kuwa njia ya kuishi tu hadi kuwa biashara yenye faida na heshima kwa kila mtu.
Nguvu ya mpango huu ipo katika kuendeleza ushirikiano na ujumuishi, unaonufaisha wakulima kupitia mikutano ya mara kwa mara na wataalamu wa kilimo pamoja na kubadilishana maarifa, huku ukisisitiza upatikanaji wa mazao kwa njia rasmi kupitia mikataba.
Mpango wa Shamba ni Mali umeundwa kuendana na Mpango Mkakati wa Taifa wa Kilimo 2030, unaolenga kujenga sekta ya kilimo thabiti, wenye kustahimili na faida. Usalama wa chakula nchini Tanzania unategemea moja kwa moja utendaji wa wakulima, na kwa kuwawezesha kwa kuwapa maarifa, zana za kisasa, na soko, SBL inaunda jukwaa la kuhakikisha kilimo kinaendelea kuwa thabiti licha ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi na soko.
Mpango huu si wa kawaida; ni mfano wa mageuzi katika uchumi wa vijijini na mradi wa urithi wa muda mrefu, unaolenga kubadilisha kilimo kutoka njia ya kuishi tu hadi kuwa biashara yenye faida na heshima kwa wakulima wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...