
Waipongeza kwa kuwafungulia barabara wakulima
Dodoma
Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI wakiongozwa na Mhandisi Rogatus Mativila Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Sospeter Mtwale - Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI) na Prof. Tumaini Nagu - Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea Banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.
Makatibu Wakuu hao wamepatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa Wakala huo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Bi. Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango ya TARURA inayohusu uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Naibu Katibu Mkuu Sospeter Mtwale amewapongeza TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kufungua barabara hususan maeneo ya wakulima,wavuvi na wafugaji na hivyo kuwarahisishia kusafirisha mazao yao.
Pia amesema barabara hizo zimesaidia waendesha bodaboda na waendesha vyombo vya moto vingine na hivyo kupata ajira hivyo kuwataka kuendelea kuboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika wakati wote.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...