Na Albert Thomas Kawogo
TAASISI ya Marian Schools Bagamoyo imeandaa mbio za marathon MARIAN SCHOOLS MARATHON 2025 zitakazofanyika Bagamoyo Ijumaa ya tar 15 Agosti
Msemaji wa Marian Schools Ohsana Mnalunde amesema mbio hizo zitaanzia kwenye kijiji cha Zinga Samakisamaki na kumalizikia kwenye hoteli ya Stella Maris Bagamoyo mjini.
Mnalunde amesema tayari zaidi ya washiriki 5000 wamethibitisha ushiriki wao huku idadi kubwa ya watu wa Bagamoyo ikionyesha nia ya kushirki mbio hizo
Msemaji huyo amesema mgawanyo wa mbio hizo ni wa km 21,km 10 na km 5 ambapo idadi ya washiriki watarajiwa ni wanafunzi,wazazi, wafanyakazi,walimu na wakuu wa mashrika ya serikali na binafsi pamoja na wafanyakazi wao
Naye Meneja wa Taasisi za Marian Schools Padre Valentine Bayo amewataka watu wengi kujitokeza kujisajili ili waweze kushiriki kwani kukimbia ni afya na kunasaidia kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoyakuambukiza kama shinikizo la damu sukari na moyo.
Padre Bayo ambaye pia ni mwanzilishi wa shule za Marian amesema watu wanaingia gharama kubwa kutibu magonjwa yatokanayo na uzito wa kupindukia lakini kama wangejenga utamaduni wa kufanya mazoezi hasa kukimbia wangeepuka magonjwa hayo.
Mbio hizo ambazo kwa mwaka huu zinatimiza miaka mitatu sasa zimedhaminiwa na Benki ya KCB.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...