Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo, amekutana na Mapostamasta Wakuu Wastaafu katika kikao maalum kilicholenga kubadilishana uzoefu juu ya namna ya kuendelea kuboresha huduma za Posta nchini.

Kikao hicho, kilichofanyika leo tarehe 13 Agosti, 2025 Makao Makuu ya Posta jijini Dar es Salaam, Bw. Mbodo amesisitiza umuhimu wa kuheshimu na kuenzi historia na mchango wa Viongozi waliolitumikia Shirika, huku akieleza kuwa uzoefu na hekima yao ni hazina kubwa kwa kizazi cha sasa kinachoendeleza mapinduzi ya kisekta ndani ya Posta.

Wastaafu hao wamepongeza mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya Shirika chini ya uongozi wa Bw. Mbodo, aidha wametoa mapendekezo mbalimbali kwenye maeneo ya kuboresha huduma, kuimarisha miundombinu ya Posta, matumizi ya TEHAMA pamoja na usimamizi bora wa Rasilimali Watu.

Postamasta Wakuu wastaafu waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Deos Kh. Mndeme, Postamasta Mkuu ( 2008-2015 ), Fortunatus Kapinga Postamasta Mkuu ( 2015 - 2017 ), Deogratius C. Kwiyukwa Postamasta Mkuu ( Machi 2017 - Novemba 2017 ), Hassan Mwang’ombe Postamasta Mkuu ( 2017 - 2021) pamoja na Maharage Chande Postamasta Mkuu (Septemba 2023 - Julai 2024).

Shirika la Posta linaendelea kuimarisha huduma zake kwa kutumia teknolojia, kushirikiana na wadau mbalimbali, huku likienzi na kutumia maarifa ya watumishi waliotangulia ili kufanikisha mageuzi endelevu.














Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...