Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema jeshi hilo linatekeleza kikamilifu maelekezo ya viongozi wa kitaifa ikiwemo ya kutakiwa kuendelea kuonesha shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi zinazofanywa na JKT hata baada ya maonesho ya wakulima (Nanenane) kuhitimishwa Agosti 8, 2025. Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Agosti 4, 2025 alipotembelea eneo la JKT katika viwanja vya maonesho ya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma ambapo amesema JKT imejenga miundombinu ya kudumu kwenye eneo lao, hivyo wapo katika eneo hilo mwaka mzima, sio wakati wa maonesho ya Nanenane pekee.

Mkuu huyo wa JKT ambaye ametembelea maeneo mbalimbali kama eneo la mifugo, mabwawa ya samaki, vipando (mashamba darasa) pamoja na zana na teknolojia za kilimo, amewahimiza Watanzania kutembelea eneo la JKT na maonesho ya Nanenane kwa ujumla ikiwemo katika mabanda ya jeshi hilo katika maonesho yanayoendelea katika kanda mbalimbali nchini ili kupata elimu ya namna jeshi hilo limejikita katika kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...