NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Wachambuzi wa masuala mbalimbali wamehimizwa kufanya tafiti ya kutosha kabla ya kufanya chambuzi zao ususani linapokuja suala la utekelezwaji wa miradi inayosimamiwa na Serikali ili kuepusha upotoshaji kwenye jamii 

Hayo yamesemwa leo Agosti 30, 2025 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPPC), David Kafulila wakati wa mdahalo maalum ulioratibiwa na Jukwaa la Wachambuzi, ambao ulikuwa na mada isemayo mwenendo wa uchumi wa awamu ya sita na nafasi ya sekta binafsi na umma katika ujenzi wa uchumi jumuishi.

Aidha Kafulila amesema katika maendeleo ya nchi yoyote duniani uadilifu ni suala muhimu na la kuzingatiwa sana ili kufikia malengo ya kitaifa.

Amesema ni muhimu zaidi kila mwananchi kuzingatia suala la uadilifu katika sekta zote zinazogusa uchumi wa taifa, huku akihadharisha kwamba rushwa na matumizi mabaya ya malighafi za taifa zinarudisha nyuma kasi ya maendeleo.

"Ni muhimu na lazima kuwa na watu wenye maarifa, uadilifu na bidii. Hivi vitu vitatu ndio vinaamua uimara wa watu kuanzia ngazi ya familia ipande kwenye kijiji, kata mpaka taifa". Amesema Kafulila 

Baadhi ya wachambuzi wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika kutekeleza majukumu yao 









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...