Na Oscar Assenga,TANGA

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imebamiza Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli mabao 3-2 katika michuano ya Shirikisho la Michezo la Mamlaka za Serikali za Mitaa kaika mchezo uliochezwa kwenye viwanja vya Shule ya Ufundi Tanga.




Shirikisho hili la Michezo linahusisha watumishi waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ( Halmashauri) waliopo kwenye idara na vitengo mbalimbali.Katika mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu kutaka kupata ushindi lakini Halmashauri ya wilaya ya Muheza iliweza kuhimili na kuutawala vyema mchezo huo na hatimaye kuweza kuibuka na kidedea

Mashindano ya Shirikisho la Serikali za Mitaa Tanzania ( SHIMISEMITA) yalianza rasmi Agosti 15, 2025 na yanatarajiwa kukamilika Agosti 29, 2025 huku yakilenga kuwakutanisha watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kushirikiana pamoja, kufahamiana, kubadilishana mawazo, kujenga Afya za watumishi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo kisukari na shinikizo la damu.

Michezo hii inaendelea katika Viwanja mbalimbali vya Michezo vilivyopo Jijini Tanga huku yakiwa yamebeba Kauli mbiu ya SHIMISEMITA 2025 " Jitokeze kupiga Kura kwa maendeleo ya Michezo".


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...