Katika kuendeleza juhudi za kuimarisha uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za Wanyamapori, Taasisi ya Caribbean Naples Zoo kutoka Nchini Marekani imetoa msaada wa mahema kumi (10) kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine waliopo katika eneo la urithi wa dunia la Ngorongoro.
Mwakilishi wa Caribbean Napple Zoo Tanzania Albert Mollel ameeleza kuwa taasisi yao kusaidia vitendea kazi hivyo ni muendelezo wa ushirikiano katika kuimarisha ulinzi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za wanyamapori hasa adimu na waliopo hatarini kutoweka kama Faru.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Kamishna wa Uhifadhi NCAA Bw. Abdul-Razaq Badru ameishukuru Caribbean Naples Zoo kwa msaada huo muhimu na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitawawezesha askari wa uhifadhi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika ulinzi wa Faru na wanyama wengine waliopo Hifadhi ya Ngorongoro pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...