NA MWANMDISHI WETU, MKURANGA
KUELEKEA Mitihani ya Taifa ya mwisho wa mwaka kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini, Benki ya NMB imewataka wazazi na walezi kujikita katika ujenzi wa msingi imara wa kesho iliyo bora kwa watoto wao, kwa kuwazoesha utamaduni chanya kuweka akiba kwa ustawi na maendeleo ya kielimu na kimaisha.
Wito huo umetolewa na Meneja wa NMB Tawi la Mkuranga, Godwin Manimo, wakati wa Mahafali ya tatu na ya tano ya wanafunzi wa Kidato cha Nne na Darasa la Saba wa Shule za Sekondari na Msingi za Al-Rahmah, zilizo Mkuranga mkoani Pwani, zikiwa chini ya Kituo cha Maendeleo cha Al-Rahmah Development Complex.
Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba inayoandaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itafanyika Septemba 10 na 11 mwaka huu, huku ile ya Kidato cha Nne ikitarajiwa kuanza Novemba 10, 2025, ambako wanafunzi wa Al-Rahmah wataungana na wenzao kote nchini, kuhitimisha hatua moja kielimu, kabla ya kuanza nyingine 2026.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, yaliyodhaminiwa na NMB kupitia Akaunti za Mtoto na Chipukizi, Manimo aliwapongeza wazazi na walezi kwa upendo wa dhati, uwekezaji mkubwa kielimu na uwajibikaji wao kwa watoto katika kutimiza malengo ya vijana wao, walio kwenye mikono salama ya shule za Al-Rahmah.
“NMB tumedhamini mahafali haya kama ishara ya kuunga mkono juhudi za Al-Rahmah Complex, kuunga mkono uongozi wa shule hizi, ambao unafanya kazi kubwa, lakini pia kusapoti jitihada za walimu, ambao wanatoa maarifa chanya kwa watoto hawa, halikadhalika kwa wafanyakazi wengine wa Al-Rahmah ambao si walimu.
“Pamoja na kuunga mkono, kutambua na kuthamini kazi zenu, tumekuja hapa na masuluhisho maalum kwa watoto wetu, tumewaletea bidhaa mbili rafiki kwa vijana hawa, ambazo ni ‘NMB Mtoto Account’ na NMB Chipukizi Account,’ ambazo ni hatua muhimu katika kuanza safari ya malengo na kuwajengea watoto utamaduni chanya wa kuweka akiba.
“Hizi ni akaunti bora kabisa katika kuweka mipango ya akiba kwa watoto wetu, kila mzazi hapa anapaswa kutambua siri hii, kwamba wakati unatimiza malengo ya mwanao kielimu mwaka huu, utakuwa unahitaji fedha katika kutimiza malengo yao yajayo kielimu kuanzia mwakani.
“NMB Mtoto Account na NMB Chipukizi Account, ndio mshirika sahihi katika kuyatimiza malengo hayo kwa watoto wanaoishia umri wa miaka 13 na wanaoanzia miaka 13 hadi 18,” alisema Manimo, mbele ya Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo, Omary Said Msumba, ambaye ni Mtakwimu wa NECTA.
Katika mahafali hayo, NMB ilitoa zawadi ya kuwafungulia akaunti Wanafunzi 10 - Walioshika Tano Bora ya Ufaulu wa mitihani ya ndani kwa Darasa la Saba na Kidato cha Nne, na kuwawekea akiba ya Sh. 80,000 kila mmoja, huku wanafunzi 64 wa kwanza wakifunguliwa akaunti za Mtoto na Chipukizi bure na kuwekewa akiba ya Sh. 10,000 kila mmoja.
“Baada ya ufunguzi wa akaunti hizi kwa watoto hawa, kazi inabaki kwa wazazi kuanza kuweka malengo ya fedha kwenye akaunti za watoto wao. Malengo hayo tunaamini hayatakuangusha mzazi, kwani ukianza kuweka akiba kidogo kidogo kila mwezi, basi mwisho wa mwaka hautopata tabu ya kutafuta ada.
Katika kuhakikisha shule za Al-Rahmah zinaendelea kuwa na ufaulu mkubwa na kitovu cha maadili, Mkurugenzi wa Al-Rahmah Complex inayofanya kazi chini ya Taasisi ya African Relief Organisation kwa msaada wa Al-Rahmah Global ya Kuwait, Dk. Ally Abdulgaffar, alitoa ahadi tatu kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wake.
“Ahadi ya kwanza ni kuwa, Al-Rahmah Schools zitakuwa shule za kwanza kabisa nchini kuingiza Mafunzo ya Awali ya Teknolojia ya Akili Unde (AI), ambayo majaribio yake yataanza hivi karibuni kwa wanafunzi wa wanaojiandaa kuanza kidato cha kwanza ‘pre-form one’ mwakani 2026,” alisema Abdulgaffar.
Ahadi ya pili ya Mkurugenzi huyo ni kuanzisha Programu ya Kuzalisha Mabalozi wa Al-Rahmah, ambao ni wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne na Sita, kwenda kuyatangaza maadili mema ya shule zake katika jamii, pamoja na ujio wa Programu ya Kuandaa Viongozi ‘leadership programme,’ ili wanafunzi wawe weledi wa uongozi wanapomaliza masomo yao.
Mtakwimu wa NECTA, Msumba, yeye aliupongeza uongozi wa Al-Rahmah Schools kwa kufanya kazi kubwa ya kuelimisha watoto katika Elimu Dunia na Elimu ya Dini, lakini zaidi kwa kulifanyia kazi wazo aliloliita ni ‘hot cake’ la kuanza Mafunzo ya Awali ya Teknolojia ya Akili Unde (AI) shuleni hapo.
“Nilipokuwa nakuja, moja ya vitu ambavyo nilifikiria ni pamoja Akili Unde, nimefika hapa nimekuta nyinyi mmeianza kwa levo ya shule za msingi na sekondari, hicho mnachofanya ni kujiongezea thamani kwa Serikali, kwamba ninyi ni ‘wawekezaji serious’ mnaopaswa kuongezewa nguvu katika kuutengeneza umma wa Kitanzania kielimu.
“Artificial Intelligence ni ‘hot cake, either you go with it or you die.’ Haiwezekani kwa ulimwengu tulionao sisi kwenda mbele kimaendeleo bila Akili Unde, hatutoweza. Kwahiyo hongera kwa uongozi, kwani wakati Serikali inapanga kufanya, ninyi mko mbele zaidi,” alisema Msumba na kusema Serikali imepata pa kujifunza ndani ya nchi tu.
Katika Risala ya Shule hiyo iliyosomwa na Mwanafunzi Faiz Abdulmalick Feruzi, waliishukuru NMB kwa kudhamini mahafali yao, huku wakitoa ombi kwa Mgeni Rasmi na Wadau wa Elimu nchini kusaidia changamoto za uhaba wa makazi ya walimu, viwanja vya michezo, vifaa vya kujifunzia na ufadhili wa vipaji maalum vya wanafunzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...