HATIMAYE makundi ya watia nia wa kiti cha udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Pugu wilayani Ilala,jijini Dar es Salaam yamevunjwa rasmi leo kwa watia nia ambao kura za maoni hazikutosha kumuunga mkono mgombea Udiwani wa kata hiyo Frank Mang'ati.

Mkutano Chama wa kuvunja makundi hayo umefanyika leo ambapo ulihudhuriwa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, ambaye katika uchaguzi wa ndani wa CCM kura zake hazikutosha.

Aliyekuwa mtia mwingine ambaye alihudhuria kikao hicho ni Magere Paul ambapo kwa pamoja walikubaliana kumuunga mkono Mang'ati na kuhakikisha CCM inashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Katika hotuba yake, Mgombea Udiwani wa Kata ya Pugu, Mang'ati, amesema ni wakati wa Wana CCM katika kata hiyo kushikamana kuhakikisha anashinda.

Pia Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Samia Suluhu Hassan, kuhakisha anapata ushindi wa kishindo.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...