Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu amesema kwa jinsi ambavyo wananchi wanajitokeza kwa wingi katika mikutano yake wale waliokuwa na maswali sasa watakuwa wameanza kutafuta.
Ametoa kauli hiyo leo Agosti 31,2025 alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa Mkoa wa Dodoma ambao walifika kumsikiliza akinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu sambamba na kutoa muelekeo wa Serikali atakayoiunda baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Wakati akihutubia wananchi wa Dodoma Dk.Samia amesema kwamba Dodoma wamethibitisha mkoa huo ndiyo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi.
"Dodoma tangu nilipoingia jana kule Kibaigwa, leo nimetoka Chemba, Kondoa na hapa Dodoma Manispaa, Dodoma mmefunika. Dodoma CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo nyinyi. Hapa wale wenye maswali nadhani sasa kidogokidogo wanaanza kufuta, wale wenye kujiuliza nadhani wanaanza kufuta.
"Kwa umma huu, CCM oyeee....niwashukuru sana ndugu zangu wa Dodoma kwa mapokezi haya kwa kweli mmethibitisha kwamba, hapa ndiyo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi, mmethibitisha na mmembeba mgombea wenu, mkazi wa Chamwino hapa Dodoma, nawashukuru sana ndugu zangu.”
Pamoja na hayo Rais Dk.Samia ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kuchapakazi huku akieleza mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake.
Akieleza zaidi Dk.Samia amesema kuwa katika Serikali ya Awamu ya Tano walifanya uamuzi wa kuhamia Dodoma, hivyo Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza kuhamia Dodoma,l na kwa sasa tayari taasisi zote za serikali zipo Dodoma, maamuzi yote makubwa sasa yanafanyika hapa.
Hata hivyo akielezea kuhusu Mkoa wa Dodoma amesema kuwa Serikali imemimina fedha Sh.trilioni 9.5 kwa miradi 3,093 ndani ya Mkoa huo na kuongeza pamoja na kuongeza majengo na kuipa hadhi Hospitali ya Benjamin Mkapa, wilaya za Dodoma zina hospitali za kisasa ambazo vipimo vyote vinapatikana huko.
Amesema pia Serikali imejitahidi kufungua fursa za ajira kupitia uwekezaji kwa kujenga viwanda, kutengeneza fursa kwa wafanyabiashara wadogo huku mradi wa reli ya kisasa (SGR) ukiongeza kasi ya ukuaji uchumi.
Akizungumzia umeme, ameeleza kwamba Serikali inandelea na kazi ya kumalizia vitongoji ili kila mtu apate nishati hiyo kufanyakazi na kulinda usalama wao.
Pia amesema Serikali imejipanga kutatua uhaba wa maji kwa kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria na kumalizia ujenzi bwawa la Farkwa kusaidia kuleta maji Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...