Na mwandishi wetu,Dodoma

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika uwezeshaji wakulima kwa kuwapatia mikopo ya Pembejeo.

Akitoa maelezo kwa Mhe. Rais Samia kuhusu utendaji wa Benki hiyo leo Agosti 8,2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Nane Nane kitaifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw.Frank Nyabundege amesema mtaji wa Benki hiyo umekuwa kutoka bilioni 60 hadi bilioni 442.

"Benki yetu itaendelea kudhamini maonesho ya NnNe Nane kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kwa sababu imeiwezesha kuwa na mtaji mkubwa," alisisitiza Nyabundege.

Mgeni rasmi katika maonesho ya Nane Nane Kitaifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...