Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kibaigwa


MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi((CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameendelea na mikutano yake ya kampeni za kuomba kura katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu na akiwa Kibaigwa wilayani Kongwa katika Mkoa wa Dodoma aliamua kujipiga picha huku nyuma yake kukiwa na maelfu ya wananchi.


Tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni ya Dk.Samia Suluhu Hassan maelfu ya wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa ajili ya kumsikiliza anavyoinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025-2030 sambamba na kusikiliza ahadi zake kwao.

Hata hivyo mkutano wa Kibaigwa uliofanyika jioni wakati Dk.Samia akitokea Mkoa wa Morogoro kuelekea Dodoma umeendea kudhihirisha mapenzi wwliyonayo wananchi kwa Rais Samia ambaye katika uongozi wake kwa kutumia falsafa ya R4 watanzania wanafurahia matunda ya maendeleo huku nchi ikiendelea kuwa yenye umoja,upendo na mshikamano.

Akiwa katika mkutano huo  wa Kibaigwa, Dk.Samia Suluhu Hassan ameahidi katika miaka mitano ijayo anaendelea kuleta mabadiliko makubwa kwa wana Kibaigwa hivyo kukibwa ni kumpa kura katika Uchaguzi Mkuu.

“Niwakumbushe tu Julai mwaka 2021 nilikutana na wanakongwa wakiwa na mbunge wao hayati Job Ndugai na wakati ule kulikuwa na changamoto nilizoelezwa na niliahidi nitaendelea kuleta fedha kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hili na leo wote ni mashahidi,” amesema

Kuhusu sekta ya  sekta ya elimu Dkt Samia ameeleza kwamba mbali na  ujenzi wa shule za msingi na sekondari Serikali imekamilisha ujenzi wa chuo cha Veta kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 2 ,hivyo vijana wanapata ujuzi ambao utawawezesha kuajiriwa na kujiajiri.

Ameehadidi kuendelea na mpango wa Serikali wa elimu bila malipo sambamba na kuendelea na ujenzi wa miundombinu katika sekta ya elimu nchini.

Wakati kwa upande wa sekta ya afya amesema kuna mambo Mengi yamefanyika na huduma zimeboreshwa sambamba na kuongeza vituo vipya 14 na sasa kuna jumla ya vituo 73.

“Hii ni pamoja na kuongeza majengo 14 mapya ikiwemo jengo la huduma za dharura katika hospitali ya wilaya yenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 pamoja na vifaa tiba vya kisasa”

“Kituo cha afya cha Kibaigwa hapa sasa kinatoa huduma mpaka za Xray na tumeleta mashine ya Xray mpya na ya kisasa huduma ambazo wananchi wa Kibaigwa walikuwa wazifuate Dodoma mjini sasa zinapatikana hapa Kibaigwa” amesema

Ameongeza kwamba Vijiji vyote vya Kongwa vina umeme na tunaendelea na kazi ya kusambaza umeme kwenye vitongoji kwenye taasisi na majumbani kwa watu.

Hata hivyo amewaahidi kufanya makubwa zaidi katika Wilaya ya Kongwa katika miaka mitano ijayo hivyo amewaomba wananchi hao kuchagua wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu ili kazı ya kuleta maendeleo iendelee.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...