Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kwasasa Ushirika umeimarika kwakuwa na Mifumo ya kisasa ya kidigitali ambayo inachangia uwazi katika utendaji wa Vyama vya Ushirika.
Mhe. Senyamule amebainisha hayo Agosti 6, 2025 wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya Vyama vya Ushirika katika kijiji cha Ushirika kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane Jijini Dodoma.
"Nilipotembelea mabanda nimefurahishwa sana kuona Ushirika upo kidigitali, hii itawawezesha wanaushirika kuwa sehemu ya Usimamizi kwakuwa taarifa za Vyama zitapatikana kwa uwazi na haraka," amesema Mhe. Senyamule.
Aidha, amepongeza Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC) pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuandaa Kijiji cha Ushirika na kuwaleta wanaushirika pamoja .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...