Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkundo wa Juu wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni amesema kuwa sekta ya gesi asilia na sekta ya kilimo ni sekta zinazotegemeana kwa karibu na kwamba sekta hizi zikifungamanishwa vizuri zitaongeza tija katika uchumi.
Sangweni ameyasema hayo Agosti 07, 2025 alipotembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Sangweni alibainisha kuwa, gesi asilia inayozalishwa nchini inaweza kutumika kama malighali kuzalisha ammonia, kemikali ambayo hutumika kuzalisha mbolea za aina mbalimbali ikiwemo urea.
Alieleza pia kuwa, matumizi ya gesi asilia kwenye magari yamesaidia kupunguza gharama za uendeshaji hivyo gesi asilia ikitumiwa katika magari yanayosafirisha mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji.
Kwa upande mwingine, Sangweni alieleza kuwa sekta ya kilimo imeendelea kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya mafuta na gesi asilia kwa kulisha wataalamu wanaofanya kazi katika miradi ya mafuta na gesi asilia nchini.
Pamoja na sekta ya kilimo kutoa huduma hii muhimu, Sangweni alisema bado kumekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo kampuni hususan kampuni za nishati za kimataifa kuhitaji bidhaa za kilimo zenye ubora na viwango ambavyo watoa huduma wachache wakitanzania wanakidhi.
Hata hivyo, Sangweni alibainisha kuwa, PURA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa viwango na ubora hitajika vinafikiwa kwa maslahi mapana ya uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...