Stanbic Bank Tanzania imeeleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuchochea ustawi wa kiuchumi kupitia ufadhili wa miradi mikubwa ya kimkakati na upatikanaji wa mikopo yenye masharti nafuu, ikiwemo riba chini ya viwango vya kibiashara.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Tanzania, Bw. Manzi Rwegasira, mbele ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wakati wa hafla ya kufunga Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha.
Bw. Rwegasira alisema: “Tukiwa sehemu ya Standard Bank Group, benki kubwa zaidi barani Afrika, Stanbic Bank ambayo imehudumu nchini kwa miaka 30 imejipambanua kama chachu ya ukuaji wa uchumi wa taifa kwa kutoa suluhisho za kifedha bunifu, ushauri wa uwekezaji, na mikopo nafuu inayounganisha fursa za ndani na mitaji ya kimataifa.”
Wakati wa hafla hiyo, Stanbic Bank ilipokea cheti cha kutambua nafasi yake kama mdhamini wa kikao kazi hicho kutoka kwa Mhe. Dkt. Biteko.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao kazi hicho, Kwa Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Stanbic Bank, Ester Manase alieleza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita, Benki hiyo imetoa mikopo nafuu ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni moja kufadhili miradi ya kimkakati nchini.
“Tunashukuru kwamba uwezo wetu katika eneo hili unatambulika ndani na nje ya Tanzania. Hivi karibuni, tulitunukiwa tuzo ya Benki Bora ya Uwekezaji Nchini (Best Investment Bank) na jarida la kimataifa la EuroMoney; ikiwa ni mara ya tano mfululizo kupokea heshima hiyo,” alieleza.

Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mbele kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Ester Manase wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye kongamano la Wenyeviti na Watendaji wakuu wa taasisi za umma nchini linaloendelea jijini Arusha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...