Na Diana Byera, Bukoba
Katika Maonesho ya Nane Nane mwaka 2025, Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) imetoa mafunzo kwa wakulima wa kahawa mkoani Kagera kuhusu Amri Nane za Kilimo Bora cha Kahawa, lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji na kufikia lengo la taifa la kuzalisha tani 200,000 za kahawa safi ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza katika banda la TACRI, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Kanda ya Kagera, Dkt. Nyabisi Ngh’oma, alisema kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2006 ulionyesha kuwa endapo mkulima atazingatia kanuni na Amri hizo, mche mmoja wa kahawa unaweza kuzalisha kati ya kilogramu 2.5 hadi 3.5 za kahawa safi.
“Leo hii tuna wakulima wachache wanaovuna hadi kilo 4 kwa mche mmoja, lakini wengi bado hawazingatii kanuni bora za kilimo. Maonesho ya mwaka huu tumeyatumia kama darasa maalum kwa kila mkulima anayetembelea banda letu ili ajifunze na kuanza kuzalisha kwa tija zaidi,” alisema Dkt. Ngh’oma.
Aliongeza kuwa kabla ya kuanza kwa jitihada hizo mwaka 2021, baadhi ya wakulima walikuwa wakivuna gramu 300 tu kutoka kwa mche mmoja, hali ambayo ilisababisha mkoa wa Kagera kupoteza mapato mengi. “Kupitia mafunzo haya, tunatarajia kuona mabadiliko makubwa kwa wakulima wote wa kahawa,” alisisitiza.
Dkt. Ngh’oma alisema kuwa hadi sasa Kagera ina zaidi ya miche milioni 51 ya kahawa, na endapo wakulima wote watazingatia kanuni bora, mkoa unaweza kuvuna hadi tani 127,000 za kahawa safi kwa mwaka, na hivyo kuingiza mabilioni ya fedha ambazo zinaweza kuinua maisha ya wakulima na kukuza uchumi wa ndani.
Aidha, alitaja changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kuwa inathiri uzalishaji, hasa kutokana na kuchelewa kwa mvua, hali inayosababisha kushuka kwa ubora wa kahawa aina ya ndagashe, na hivyo kuathiri bei sokoni.
Amri Nane za Kilimo Bora cha Kahawa, ni Kukata matawi vizuri kusaidia mmea kutoa matawi yenye tija, Kudhibiti magonjwa na wadudu kulinda afya ya mmea, Kuweka mkazo kwenye lishe ya miti ya kahawa kutoa virutubisho vya kutosha, Kufanya palizi shambani kuondoa magugu yanayonyonya virutubisho.
Kuondoa maotea mara kwa mara kupunguza ushindani wa lishe, Kuweka matandazo vizuri kuhifadhi unyevunyevu na kupunguza mmomonyoko wa udongo, Kumwagilia maji inapobidi hasa wakati wa jua kali,
Kupangilia kivuli kwa ushauri wa wataalamu kuhakikisha mmea unapata mwanga na kivuli kwa uwiano sahihi.
Katika banda la TACRI, wakulima walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo kupitia shamba darasa lililoandaliwa ndani ya eneo la maonyesho, pamoja na kufurahia kahawa ya bure kama njia ya kuhamasisha matumizi ya kahawa na kuongeza thamani ya zao hilo.
Kupitia vijiwe vya kunywa kahawa vinavyoanzishwa, TACRI inalenga kuchochea uanzishwaji wa biashara ndogo ndogo za kahawa na kukuza uchumi wa wakulima wa zao hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...