Meneja Mara aomba ushirikiano wa walipakodi ili kuvuka lengo hilo
Awashukuru walipakodi kwa ushirikiano wao
Na. Mwandishi wetu
Mara
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara Bw. Nasoro Ndemo ametaja lengo la makusanyo mkoani humo kwa mwaka huu wa fedha 2025/26 kuwa ni shilingi bilioni 208 na kuomba ushirikiano wa walipakodi wa mkoani humo ili kuvuka lengo hilo.
Akizungumza wakati akifungua semina ya mabadiliko ya sheria ya kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26, Bw. Ndemo ameeleza kuwa, lengo hilo litafanikiwa iwapo wataendeleza ushirikiano baina yao na TRA kama ambavyo ushirikiano huo ulivyowafanikisha kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2024/2025
“Kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru walipakodi na wadau wote mliotufanikisha kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka uliopita na ninawaomba ushirikiano huu uendelee ili tuweze kuvuka lengo tulilopangiwa kwa mwaka huu ambalo ni shilingi bilioni 208 ambapo upande wa ushuru na forodha lengo ni shilingi bilioni 146 na kodi za ndani ni shiligi bilioni 61”, alisema Meneja Ndemo.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mara Bi. Phelister Nyambaya amewasisitiza walipakodi waliohudhuria semina hiyo kufuatilia kwa makini ili waweze kupata uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya sheria ya mwaka huu kwa lengo la kuwasaidia kwenye kazi zao za kila siku.
“Semina hii ni muhimu sana kwetu sisi wafanyabiashara hivyo nawaomba tufutilie kwa makini elimu hii ya mabadiliko ya kodi kutoka kwa wenzetu wa TRA ili tupate uelewa wa kutosha na hatimaye tumweze kulipa kodi stahiki,” alieleza Bi. Nyambaya.
Kwa upande wake Mshauri wa Fedha kutoka Dayosisi ya Musoma mkoani Mara Bw. Moses Kimwaga ameishukuru TRA kwa kuendesha semina ya mabadiliko ya sheria na kuiomba kuanzisha kitengo cha kuhudumia makundi maalumu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu ya kodi kwenye makundi hayo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania ina utaratibu wa kutoa semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kila baada za kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa watumishi wa TRA, wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika mikoa yote nchini.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara Bw. Nasoro Ndemo akifungua semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 mkoani Mara. Kulia kwake ni Bi. Pherister Nyambaya ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa humo.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mara Bi. Pherister Nyambaya na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara Bw. Nasoro Ndemo wakiteta jambo wakati wa semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa walipakodi wa mkoani Mara.
Baadhi ya Walipakodi waliohudhuria semina ya elimu kwa Walipakodi juu ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 iliyofanyika leo mkoani Mara.
Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Eugenia Mkumbo akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 katika semina iliyofanyika leo mkoani Mara.
Baadhi ya Walipakodi waliohudhuria semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa walipakodi iliyofanyika leo mkoani Mara.
Baadhi wa watu wenye mahitaji maalumu ambao ni viziwi wakiwa pamoja na mkalimani wao Bi. Fatuma Selemani wakiwa wanasikiliza semina ya mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2025/26 kwa walipakodi iliyofanyika leo mkoani Mara.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...