Na.VERO IGNATUS ARUSHA
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imezindua mfumo wa maarifa (knowledge management system) unaolenga kuongeza ufanisi,uwazi,na weledi katika ukusanyaji wa mapato ,sambamba na kuboresha huduma kwa walipa kodi katika mazingira ya sasa ya biashara yenye ushindani mkubwa yanayochochewa na teknolojia na utandawazi.
Yusuphu Mwenda ni Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesema kuwa mfumo huo unafaida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhifadhi taarifa za watumishi wanaostaafu,kukuza maendeleo ya kitaaluma kwa watumishi,uboreshaji wa maamuzi kwa kutumia taarifa sahihi za kisasa, kupunguza gharama kwa kuondoa marudio ya kazi ,mapungufu ya kiutendaji kuongeza ufanisi na tija kwa kupitia taratibu zilizorahisishwa.
Mwenda amesema kuwa kuzinduliwa kwa mfumo huo ni utekelezaji wa moja ya maagizo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoipa mamlaka hiyo kukusanya kodi kwa kuwatendea haki walipa kodi na kuepuka kuwawekea makadirio makubwa kiliko yanayostahili,huku akisisitiza vitu vinavyoweza kusababisha kutokutenda haki ni pamja na kutokuwa na maarifa.
‘’Mhe.Rais alitupa agizo Mamlaka kuhakikisha tunatenda haki kwa walipa kodi kwa kutowawekea makadirio makubwa wala madogo badala yake tuwatendee haki ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.TRA kazi yetu kikatiba na kisheria ni kukadiria kukusanya,kuhasibu mapato ya serikali, hivyo basi ili mtumishi aweze kukusanya mapato lazima awe na maarifa ya sheria za kodi mbalimbali ,maarifa ya taarifa za sehemu unayokwenda kuikagua ambazo utazitumia kufanya ukadiriaji, Alisema Mwenda.
Kwa upande wake Naibu Kamishna mkuu TRA Mcha Hassan amesema kuwa mfumo huo unaozinduliwa leo ni miongoni mwa jitihada zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo katika kuimarisha mifumo ya teknolojia ili kuongeza tija pia unalenga usimamizi maarifa ,kumbukumbu za uzoefu kwa watumishi ili maarifa yasiishie kwa mtu mmoja anapostaafu au kubadilishwa nafasi ya kazi, kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa urahisi, kufanikisha maamuzi sahihi,kushirikisha ujuzi na mbinu bora za ukusanyaji wa mapato,mijadala ya litaaluma,tafiti, rejea za kihistorina kupanua wigo wa kujifunza na kujengeana uwezo katika utendaji wao wa sikuzote.
’’Sote tunafahamu kuwa dunia ya sasa inaendeshwa na maarifa na taarifa hivyo taasisi yeyote inayoshindwa kusimamia maarifa ipasavyo inaweza ikajikuta ipo nyuma kiushindani ndani ya Taifa na hata kimataifa’’. Alisema Mcha.
Amesema kwasasa TRA inatumia mifumo mbalimbali ya taarifa inayosaidia kuongeza ufanisi kwa wakusanyaji wa mapato ukiwemo mfumo wa usajili wa walipa kodi,mfumo wa kutoa risiti za electronic,mfumo wa ushuru wa forodha,ulipaji kodi kwa njia ya kimtandao mfumo wa kodi za ndani,hivyo mfumo huo wa usimamizi wa maarifa unaunganishwa na jitihada hizo zote ili kuhakikisha taarifa uzoefu na ujuzi vinapatikana kwa urahisi ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Mkurugenzi wa usimamizi wa rasilimali watu na Utawala Moshi Kabwenge ametaja maeneo yaliyopo katika mfumo huo moduli ya kwanza ya itawawezesha watumishi wenye ujuzi unaofanana kuwa na jukwaa la kujadili changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kwenye maeneo yao kwa pamoja ,moduli ya pili ni kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu kwaajili ya rejea ,ya tatu itawawezesha watumishi kujisomea na kupata maarifa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali .
Amewahimiza watumishi wa mamlaka hiyo kuhimiza matumizi ya mfumo huo kwaajili ya urahisishaji majukumu yao pamoja na malengo na makusudi pangwa yaweze kutekelezwa sambamba na eneo la kupata maarifa kwa kutoka kwenye vyanzo urahisi .
Aidha uzinduzi huo umehudhuriwa na watendaji wa Mamlaka hiyo wakiwemo makamishana wa idara za kodi wakurugenzi wa idara saidizi manaibu makamishana na wakurugenzi wa idara na mameneja wa mikoa ambapo umefanyika katika jingo la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo barabara ya Moshi Arusha Kata ya sekei Jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...