Na Diana Byera-Kyerwa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amezindua rasmi uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ujulikanao kama Nsekela Stadium uliojengwa na Abdulmajid Nsekela Mwenyekiti wa taasisi ya Abdulmajid Nsekela Foundation.
Akizindua uwanja huo uliojengwa Wilayani Kyerwa katika eneo la Rwenkorongo Mkuu wa Mkoa Mwassa amempongeza Abdulmajid Nsekela mzaliwa wa Kyerwa kutekeleza kwa vitendo wito wake wa "Ijuka Omuka" kwa kukumbuka nyumbani na kuwekeza katika mradi mkubwa unaokwenda kuinufaisha jamii ya Wanakagera.
"Uwanja huu nauangalia kwa jicho la tatu wananchi wa Wilaya ya Kyerwa wamepata fursa ya kufanya mazoezi wakiwemo wanafunzi wa shule jirani hapa, pia taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi aidha kupitia mashindano mbalimbali tutaweza kupata burudani hapa badala ya kwenda mbali na Wilaya yetu." Alisema Mwassa.
Mkurugenzi wa Nsekela Foundation Abdulmajid Nsekela alisema kuwa uwanja huo ameujenga kupitia Taasisi aliyoianzisha mwaka 2024 ya Abdulmajid Nsekela Foundation na ujenzi wa uwanja huo ni lengo mojawapo kati ya malengo nane yaliyomfanya kuianzisha taasisi hiyo.
Akiyataja malengo nane ya taasisi ya Abdulmajid Nsekela Foundation Nsekela amesema ni Elimu, Ujasiliamali, kuwezesha vijana kiuchumi, Afya ya mama na mtoto, Uongozi, Utawala bora, Ustawi wa jamii na Michezo na burudani na kudai kuwa ameanza na michezo kwa kuwa inawaleta watu wengi kwa muda mfupi.
Ujenzi wa uwanja wa Nsekela Stadium ni uwanja wa mpira wa miguu ambao utajumuisha pia viwanja vya mpira wa mikono na kikapu ikiwa ni pamoja na eneo la mashindano ya riadha na kukamilika kwa uwanja huo utajumuisha ujenzi wa majukwaa ya watazamaji na uzio wa ukuta.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...