*Atembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake ukiwemo Mfuko wa NSSF

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake ikiwemo NSSF. Maonesho ya Nanenane 2025 yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma yana kauli mbiu isemayo: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi."

NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, elimu kuhusu kujichangia kupitia simu ya kiganganjani popote walipo, pia kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za Mifumo mbalimbali ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...