NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeiipa Kampuni ya Faima General Supply jukumu la kusafirisha abiria kutoka stesheni za SGR za Dodoma na Morogoro, ambapo huduma hiyo itaanza rasmi Septemba 15,2025.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 13,2025 Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Kampuni hiyo Msemaji wa Faima General Supply, Saphina Abraham amesema kuwa kwa Mkoa wa Morogoro, vituo baada ya stesheni vitakuwa ni Viwandani, Stendi ya mabasi ya Msamvu, Masika na Stendi ya zamani ya mabasi huku upande wa Dodoma vituo baada ya stesheni vitakuwa ni kituo cha mabasi Nanenane, Machinga Complex na Shoppers Plaza ambapo gharama za usafiri kote ni shilingi elfu tano (5,000/=).

"Tunawahakikishia Watanzania kuwa tutaendana na ubora na viwango vya TRC katika kutoa huduma bora kwa abiria wote, na pia tutachangia kukuza ajira pamoja kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo haya". Amesema

Aidha amesema kuwa huduma hiyo itakuwa na mabasi sita mkoani Morogoro na mabasi saba mkoani Dodoma yakiwemo pia mabasi ya VIP moja kila Mkoa.

Amesema watakuwa na ratiba rafiki zinazolingana na muda wa kuwasili na kuondoka kwa treni za SGR, hivyo kurahisisha mwenendo wa safari.

"Tutakuwa na ratiba rafiki kabisa, mabasi yetu kote Morogoro na Dodoma yatakuwa yanaondoka vituoni saa 3 kabla ya safari ya treni kaanza". Amesema.

Amesema kuwa kwa kuanzia tiketi zitakuwa zinapatikana katika stesheni zote za SGR yaani Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma ambapo wahudumu waliovaa sare zenye nembo ya FAIMA watakuwa katika stesheni hizo kutoa huduma.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Maendeleo ya Biashara-TRC, Frederick Massawe amesema huduma hiyo itawawezesha abiria kufurahia usafiri wa uhakika, salama na wa haraka, huku wakipanua wigo wa biashara na ajira kwa watanzania.

"Huduma hii mpya inalenga kuongeza urahisi wa usafiri kwa abiria wa SGR kwa kuwaunganisha moja kwa moja na mitandao ya barabara baada ya safari za reli ". Amesema Massawe

Amesema kuwa huduma hiyo maarufu kwa lugha ya kiingereza Shuttle, ni ushahidi wa fursa zitokanazo na uwekezaji wa Serikali kupitia mradi wa SGR, ambao sio tu unarahisisha safari za abiria na mizigo, bali pia unafungua milango kwa wadau binafsi kuwekeza ratika sekta ya usafirishaji na huduma zinazohusiana na masuala ya reli.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...