VICTOR MASANGU, KIBAHA

Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Ally Hapi (MNEC) amezindua rasmi kampeni  katika Jimbo la Kibaha vijini na kuwaomba wanachama na wananchi kumpa ridhaa  ya kuweza kuwatumikia  mgombea  wa  wa Jimbo la  Kibaha mjini Hamoud Juma kwa  kura nyingi za kishindo  ili aweze kutekeleza ilani kwa vitendo na  kwa  kuwaletea chachu ya maendeleo chanya katika nyanja mbali mbali.

Hayo ameyasema wakati mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni katika Jimbo la Kibaha Vijijini ambapo amesema kwamba  wanachama wa CCM wanapaswa kuungana kwa pamoja na kuwa na mshikamano katika kuhakikisha Octoba 29 kura zote kuanzia ngazi za udiwani, Ubunge pamoja na nafasi ya Rais lengo ikiwa ni kuhakikisha wagombea wote ambao wamechaguliwa wanakwenda kusikiliza keo na changamoto za wananchi.

Hapi amebainisha kwamba lengo kubwa la chama ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025 hadi 2030 katika kuekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Pwani  ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa viwnda vya dawa vitatavyo saba viwanja vya chuma tisa, mbolea saba, viwandavya sukari, viwanda vya sukari vitatu pamoja na viwanda vya  mafuta kumi lengo ikiwa ni kutoa fursa za ajira kwa wananchi.

"Ndugu zangu wanachama na wa ccm pamoja na wananchi katika utekelezaji wa ilani ya chama chetu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea pekee ya nafasi ya Urais  kwa hivyo kitu kikubwa ninawaomba tumpe kura nyingi za kishindo ikiwemo pamoja na mgombea wetu Hamoud Jumaa pamoja na madiwani wenzake lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbali mbali,"amebainisha Katibu Hapi.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Hamoud Juma amehahakikisha wananchi  endapo wakimchagua katika uchaguzi mkuu wa Octoba 29 mwaka huu ataleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo ujenzi wa soko jipya la kisasa ambalo litaweza kuwasaidia kwa kiwango kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.

Hamoud amebainisha kwamba katika serikali ya awamu ya sita Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa katika miradi ya kimkakati ambayo kwa kiwango kikubwa imeweza kuwapa fursa wananchi  kuweza kujikimu kimaisha pamoja na kupambana na wimbi la umasikini.

Hamoud amesema kwamba lengo alke kubwa ni kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi huo wa soko ambao ana imani utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la kungoeza kazi ya kukuza uchumi pamoja na kujiongezea kipato ambacho kitaweza kuleta mabadiliko katika suala zima la kimaendeleo.

Naye  Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewataka wanachama na wananchi wasifanya makosa hata kidogo na badala yake wawe kumpa kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan, madiwani pamoja na mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha vijiji Hamoud Juma kwa ajili ya kuweza kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Aidha Mgombe ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia chama cha mapinduzi Hawa Mchafu amesema kwamba Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa katika jimbo la Kibaha vijiji kutokana na kutenga fedha nyingi amabzo zimekwenda kuleta mageuzi katika miradi  mbali mbali ya maendeleo hivyo wanachama wanapsawa kumpa kura nyingi za kishindo yeye pamoja na Hamoud Juma pamoja na madiwani wenzake.

Uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Kibaha Vijinini  ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya msingi mtongani Mlandizi  umezinduliwa rasmi Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Ally Hapi na kuhudhuliwa na  wanachama wa CCM, viongozi mbali mbali, wananchi, wenyeviti wa mtaa , sambamba na wagombea ubunge pamoja na madiwani.

                           





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...