Kibamba, Dar es Salaam – Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angellah Kairuki, ameendelea na ziara yake ya kampeni kwa lengo la kuimarisha mshikamano na mshikikiano miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Katika ziara hiyo, Kairuki alibainisha kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha changamoto za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Alitaja changamoto za soko, maeneo ya kuzikia pamoja na barabara kuwa ndizo zinazowakabili wakazi wengi wa Kibamba.

"Nitaendeleza kasi tuliyoanza, hakuna mradi wowote utakaosimama. Nitahakikisha wananchi wa Kibamba wananufaika na maendeleo ya kweli," alisema Kairuki.

Amesisitiza kuwa dhamira yake kubwa ni kuwalipa wananchi kwa uwajibikaji, kusikiliza sauti zao na kuwapigania ili jimbo la Kibamba liendelee kusonga mbele.

Kwa mujibu wake, mshikamano wa wanachama wa CCM katika jimbo hilo ndiyo chachu ya ushindi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotarajiwa kuinua maisha ya wananchi.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...