Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Ruvuma
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo Serikali inakwenda kuufungua mkoa wa Ruvuma kuwa kitovu lakini pia ukanda mzima wa kusini (Ruvuma, Mtwara na Lindi) kuwa ukanda wa biashara.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa wa Mji wa Songea mkoani Ruvuma akiwa katika mkutano wa kampeni kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2024 ,Dk.Samia ameeleza namna ambavyo Serikali imedhamiria kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda huo.
"Kwa maana hiyo mkoa huu wa Ruvuma tayari tumekamilisha upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege Songea. Nimetua jana nimeona njia ya kurukia haipungui kilometa tatu inayoruhusu ndege kubwa kutua hapa Songea.
“Njia hiyo ya ndege imeongeza idadi ya miruko ya ndege kutoka 276 hadi miruko 463 kwa mwaka. Na idadi ya abiria 3,971 hadi abiria 20,667 kwa mwaka.Awamu ya pili ya marekebisho ya kiwanja hicho ni kujenga jengo la abiria ambalo limefikia asilimia 70,”amesema na kuongeza jengo hilo litakwenda kuvutia zaidi wasafiri kwa njia ya anga.
Dk. Samia pia amesema kuwa ujenzi wa Bandari ya Mbambabay imefikia asilimia 35 huku akieleza pia serikali imekamilisha ujenzi wa Bandari ya Ndumbi ambayo imechochea biashara baina ya Tanzania na Malawi kupitia Nkatabay hivyo kuongeza fursa za kiuchumi Ziwa Nyasa.
“Mwaka jana nilizindua barabara ya Mbinga -Mbambabay inayounganisha Bandari ya Mtwara na Mbambabay.Tunafungua ukanda huu wa Kusini ili biashara ziweze kifanyika kwa anga, barabara, maji ili Ruvuma iwe kitovu kikubwa cha biashara.
“Tunakwenda kukamilisha barabara ya Kidatu - Ifakara - Malinyi hadi Lumecha inayounganisha Ruvuma na Mkoa wa Morogoro," amesema Dk.Samia.
Aidha amesema katika kuungua mkoa huo wa Ruvuma na kuwa kitovu cha biashara Serikali katika miaka mitano ijayo inafikiria kuanzisha mradi mwingine ni reli ya viwango vya kisasa ambayo itaunganisha Mtwara hadi Mbambabay.
“Serikali ikifanikiwa reli hiyo yenye urefu wa kilometa 1,000 itaunganisha Mtwara na Ruvuma, hivyo kurahisisha usafiri kwa madini yatakayochimbwa Mchuchuma na Liganga.Tunafungua ushoroba wa kusini kwa njia zote, anga, maji, barabara na reli ili kuufanya ukanda huu uwe wa kibiashara.
Katika hatua nyingine, Dk.Samia amesema licha ya serikali kujenga barabara ya lami kilometa 10 ndani ya mji wa Songea bado msongamano wa magari yapo.
Amesema ili kuondoa msongamano wa magari amekubali ombi la mgombea ubunge wa jimbo la Songea Mjini la kuomba ijengwe barabara ya mchepuko kupunguza msongamano linakwenda kufanyiwakazi.”Tutajenga barabara ya mchepuko kuondoa foleni katika Mji wa Songea.”
Mgombea urais Dk.Samia amesema pia anatambua bado wananchi wana kiu ya barabara na madaraja. “Kipaumbele chetu tutakapoendelea ni kukamilisha miradi tuliyoianza alafu ndiyo tutashika ile mingine ambayo tumeianisha kwenye ilani ya uchaguzi.”
Kuhusu mawasiliano ya simu amesema kuna maeneo ya Mkoa wa Ruvuma ambayo mawasiliano ya simu siyo mazuri. Hivyo nalo Serikali itakwenda kulifanyiakazi kuhakikisha mawasiliano ya simu yanakuwa mazuri kwa sababu ukanda wa biashara lazima uwe na urahisi wa mawasiliano," alibainisha.
Pamoja na hayo amewaeleza wananchi hao wakati yeye akiendelea kuomba ridhaa ya kuomba kuendelea kuwatumia kuna watu wengine(wagombea)wanazunguka kama yeye ambao wananadi ilani zao.
“Lakini kila nikiwasikiliza ni yaleyale yaliyopo kwenye ilani ya chama chetu lakini ndani ya ilani ya chama cha maoinduzi tukiandika tunajua tutatekeleza kwa njia gani.Fedha itatoka wapi, vipi tutakamilisha tuliyoyaandika suala siyo kusema tutafanya lakini vipi tutafanya hilo ndilo suala muhimu.
“CCM tunasimama kujiamini na ujasiri mkubwa kuomba kura mtuchague tuendelee kuongoza serikali hii kwa sababu tumefanya mmeona na ninaamini tutaweza kufanya na mtaona.”
Katika hatua nyingine Dk.Samia ameendelea kuwahamasisha wananchi ikifika siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu waende kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM)kwa nafasi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni yeye, wabunge na madiwani wa Chama hicho ili kasi ya kuleta maendeleo ya watanzania iendelee.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...