Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga.
Dkt Nchimbi akihutubia Maelfu ya Wana kahama amesema Dkt Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndio katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa Sababu amejipambanua katika Kushughulikia kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi, pamoja na kufungua fursa kwa Watanzania.
Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini,Benjamin Lukubha Ngayiwa ,pamoja na Madiwani.
Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...