MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewahutubia Wananchi wa Longido kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Polisi, leo Ijumaa Septemba 12,2025.
Mara baada ya kuwasili eneo la Mkutano,Balozi Nchimbi alikaribishwa kwa kuvalishwa vazi la heshima la Kichifu kutoka kwa Viongozi wakuu wa kimila wa Kabila la Kimasai (Malaigwanani).
Akiwa kwenye mkutano huo,Balozi Dkt.Nchimbi alipata wasaa pia wa kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Longido ,Dkt Steven Lemomo Kiruswa pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Aidha,amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...