MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewasili mkoani Arusha leo Ijumaa Septemba 12,2025 na kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea Mkoa wa Katavi.
Mara baada ya kuwasili jijini humo,Balozi Dkt.Nchimbi ataelekea Wilayani Longido,Jimbo la Longido ambako atawahutubia Wananchi wa jimbo hilo na kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Longido ,Dkt Steven Lemomo Kiruswa pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...