*Atoa majibu ya maombi ya mgombea ubunge Makambako Daniel Chongolo kuhusu…

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Makambako

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amehutubia maelfu ya wananchi wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe huku akitumia nafasi hiyo kujibu maombi ya mgombea ubunge wa Jimbo hilo Daniel Chongolo.

Akizungumza leo Septemba 6,2025 katika Jimbo la Makambako katika mkutano wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu, Dk.Samia ameanza kwa kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi.

“Umma huu ni ishara tosha kwamba mmeturidhia na sisi tunawashukuru, ndugu zangu tumekuja kuomba kura kwa ujasiri kutokana na mambo mawili.Kwanza tuliyoyafanya nyuma kwenu Wanamakambako lakini tuliyoyapanga kuwafanyia miaka mitano jjayo.

“Na ndiyo maana tunakuja kuomba kura ,nimemkabidhi Daniel Chongolo (mgombea ubunge)kitabu kidogo cha mkoa huu na jimbo la Makambako ndani kuna mambo ambayo tumeyafanya na ambayo tutayafanya baadaye.

“Kazi yake ni kupita kuwaeleza tutafanya nini ndani ya Makambako lakini pamoja na hayo tuliyoyafanya tulishayaeleza yote ndani ya mkoa.”

Kuhusu maombi ya mgombea ubunge wa Jimbo la Makambako ameomba vituo vya kununulia mahindi. Nataka niwape habari njema kwamba ndani ya mwezi huu pengine kuanzia wiki ijayo tutafungua vituo vya kununulia mahindi ndani ya mkoa huu wa Njombe.”Sasa maeneo gani yataamuliwa lakini ndani ya mkoa huu tutafungua vituo.”

Dk.Samia amesema ombi la pili la mgombea ubunge ni kumkabidhi andiko la mradi wa umeme wa upepo hivyo amesema wasaidizi wake wapo tayari kulipokea. “Lakini niungane mradi huu unakwenda kuunga nguvu katika ajenda yetu ya nishati safi.

“Umeme wa upepo, umeme wa jua, umeme wa gesi na huu wa maji tunaoutegemea sana zote ni nishati safi na Tanzania tunaongoza kwa hilo kwenye uzalishaji wa nishati safi.Kwa hiyo tupo tayari kulipokea andiko tutalipitia na tuone linalowezekana.

“Kwenye eneo la one stop centre kwamba Makambako ni mji mkubwa wa biashara hili nalo tutakwenda kulizingatia kuweza kulifanyia kazi.

“Kwanza ni kwamba tumewataka TRA kurekebisha mifumo yao lakini la pili tumeunda tume kutushauri mambo ya kodi, tutakapopokea ripoti yao Makambako itakuwa katika centre ambayo itafikiriwa katika hayo mapendekezo ya tume kuhusu mambo ya one stope.”

Kuhusu ombi la bandari kavu ambalo nalo limetolewa na mgombea ubunge Jimbo la Makambako kwa niaba ya wananchi, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema ombi hilo watalizingatia.

“Suala lingine aliomba babdari kavu sasa hili nalo tutalizingatia kwa sababu kwenye ukanda huu nimeanza Songwe kuna bandari kavu, Mbeya nimepita wanaomba bandari kavu, Njombe wanaomba bandari kavu, labda nikifika iringa nao wataomba bandari kavu.

“Sasa hili tunakwenda nalo kuona wapi hasa tuweke bandari kavu lakini bandari ya Songwe imeshapitishwa sasa tutaona lingine litaendaje.”

Aidha amewapongeza Makambako kwamba tayari Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wameshafanya matayarisho ya awali ya ujenzi wa chuo ndani ya mkoa, serikali itatoa fedha yote ili chuo hicho kianze kujengwa.

“Fedha yake ipo tayari ni kazi tu ifanyike chuo kianze kujengwa. Lingine ni la Makambako kuwa Wilaya na lichanganya na maombi ya halmashauri nilizoombwa huko nyuma.

“Kama mnavyojua kwa muda mrefu tulizuia

Kuwa na eneo la utawala ili kupunguza gharama za utawala ndani ya serikali lakini maombi yamekuwa makubwa.Tutaangalia katika awamu ijayo wapi haswa tunatakiwa kuwa wilaya kwa hadhi zake zilivyo.

“Amejenga hoja nzuri Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe kwamba taasisi zilizopo hapa zote ni za hadhi ya wilaya bado utawala tu haujaja hapa hii hoja tutaizingatia wakati tunapanga maeneo ya utawala.Maombi yote nimeyachukua tutayafanyia kazi mengine tayari yameshaanza kufanyiwa kazi,”amesema Dk.Samia.

Pamoja na kueleza hayo mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwaomba wananchi kuichagua CCM katika Uchaguzi Mkuu unaokwenda kufanyika Oktoba 29 mwaka huu na kusisitiza katika miaka mitano ijayo Serikali imepqnga kufanya mambo makubwa ya maendeleo sambamba na kuendelea kutatua changamoto.









Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...