Na Oscar Assenga,TANGA

IDADI ya Watalii wa Ndani na Nje ya Nchi imezidi kuongezaka katika Mapango ya Kihistoria ya Amboni Jijini Tanga katika kipindi cha kutoka Watalii 8000 mpaka zaidi 19000.

Takwimu hizo ni katika mwaka wa Fedha 2024/2025 hatua hiyo imewezesha Kupata mapato ua zaidi ya Milioni 40 hali inayowezesha Kuwa Mapango yaliyo na mchango Mkubwa katika maendeleo ya Taifa Kupitia shughuli za Utalii

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhifadhi wa Mapango hayo Ramadhani Rashid wakati wa ziara ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kazita wilaya Muheza wakiongozwa na Mwalimu wao Jao Kales maarufu Mwl Pawa katika Mapango hayo ambayo ni moja ya sehemu kivutio cha Utalii kinachoelezea historia ya urithi na utamaduni na harakati za wapigania Uhuru wa Nchi

Ziara hiyo ililenga kuwapa wanafunzi hao kujifunza Kwa vitendo kuhusu historia ,urithi WA utamaduni na mambo ya kale pamoja na kujifunza shughuli za uhifadhi,Utalii na utunzaji wa mazingira.

Alisema takwimu hizo zinatokana na idadi ya Watalii mbalimbali wakiwemo wanafunzi kwenda kutembelea Mapango hayo Kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya Kihistoria

Awali akizungumza Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Hifadhi eneo la Ngorongoro Mariam Kobelo alisema mamlaka hiyo imempa hadhi ya Kuwa Balozi wa Mapango hayo Mwalimu wa Shule ya Msingi Kwazita iliyopo wilayani Muheza Kwa kuelimisha kwa vitendo elimu ya Mapango hayo.

Naye Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo Juma Omarion kwa niaba ya wenzake aliishukuru NCAA Kwa kuwapatia nafasi ya kutembelea Mapango hayo na Kutoa wito Kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao ili kujifunza kwa vitendo.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...