NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ameahidi kuboresha sekta ya afya,elimu na maji pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza wananchi.
Koka ameyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni za CCM kata ya Kibaha na kusema kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Koka amebainisha kwamba anatambua wananchi wa kata ya Kibaha wanahitaji kwa kiasi kikubwa huduma mbali mbali ikiwemo suala la upatikanaji wa maji safi na salama.
"Kitu kikubwa ambacho ninawaomba kwa dhati wananchi wa kata ya Kibaha ni kuniamini pamoja na kunipa kura ili niweze kuendelea kuwapatia maendeleo katika nyanja mbali mbali,"amesema Koka.
Kadhalika Koka amebainisha kuwa ataweka mipango madhubuti ya kuweza kuhakikisha anatengeneza na kuboresha miundombinu ya barabara.
Kwa upande wake Diwani mteule wa kata ya Kibaha Omary Bula amesema kwamba dhumuni lake ni kusikiliza kero na kutatua changamoto za wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amewaomba wanachama wa CCM pamoja na wananchi kumchagua kwa kura nyingi za kishindo nafasi ya Rais Dkt.Samia,Ubunge pamoja na udiwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...