Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mbalizi
WAKATI mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano mkoani Mbeya machifu nchini wametangaza kuchukua hatua kwa njia za kimila kuwakomesha wale wote wanaobeza maendeleo na wengine kutoa lugha chafu kwa Rais Dk.Samia.
Machifu wamesema katika mambo ambayo yanawakasirisha na kuona au kusikia Rais Samia akitukwana na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamiii na hivyo wameomba pia wenye dhamana na mitandao kuwadhibiti watu hao.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Rais Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Mlima wa Reli uliopo Mbalizi mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Machifu Mbeya Vijijini Shayo Soja wa Soko ameelezea kwamba wanakasirishwa na wote wanaobeza maendeleo na kutoa lugha za kejeli kwa Rais.
Aidha amesema machifu wanafahamu upo utaratibu wa kuzuia mambo hayo yanayoendelea katika mitandao lakini wanashangaa kwanini wanashindwa kuwadhibiti watu hao wanaombeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao.
“Lakini naomba niseme jambo moja, wewe ni Chifu Hangaya na machifu wote Tanzania ni wasaidizi wako hasira tuliyonayo ni pale tunapoona wana beza mambo mazuri na kukutukana,"amesema.
Ameongeza kwamba machifu wote walioko katika mkutano huo wa kampeni na machifu wengine wote nchini watumie mambo ya kimila ili wanaofanya mambo hayo ya kipuuzi walaaniwe.
“Nchi yetu haijawahi kupata mtikisiko hivyo huyu anaetaka kutuletea mtikisiko awe nani lazıma alaaniwe.”
Pamoja na kuonesha kukasirishwa na wanaobeza mitandaoni Machifu wa Mbeya Vijiji wapatao 270 wamemkabidhi zawadi Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo kumkabidhi fimbo kama ishara ya usalama ,mgorole Mweupe Kama ishara ya amani ili wakati wa Uchaguzi asitokee mtu wa kuuvuruga.
Hata hivyo wakati anaanza kuzungumza Chifu Shayo amesema kuwa katika miaka minn na nusu ya uongozi wa Rais Samia amefanya mambo Makubwa na wale waliokuwa wanasema hataweza sasa wanaona aibu.
Pia amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na mgombea Urais katika Uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kufika Mbalizi kwani hiyo ni heshima kubwa kwao na ndio maana hata
Machifu wamejitokeza kwa wingi.”Huko nyuma wengine walikuwa wanapita tu kwenye magari lakini Rais Samia umekuja hapa kwetu.Hii ni zawadi kubwa kwetu.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...