Na Albert Kawogo


MADEREVA wanaotumia barabara ya Bagamoyo kuelekea mikoa ya kaskazini ya Tanzania wametakiwa kuwa makini katika kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu

Akizungumza katika zoezi maalum la ukaguzi wa magari na utoaji wa elimu kwa madereva wa magari yote yanayopitia njia ya Bagamoyo Mkuu wa usalama barabarani Bagamoyo Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi ASP Aziz Zuber amesema wajibu wa kwanza wa dereva ni usalama wake na abiria watembea kwa miguu pamoja na vyombo vingine vya moto vilivyo barabarani.

ASP Zuberi amesema ajali nyingi zinaweza kuepukwa ikiwa madereva watazingatia kanuni na wajibu wao wanapokuwa barabarani.

Amesema wajibu huo ni pamoja na kuwa na leseni za chombo sahihi wanachokiendesha,kufuata sheria za barabarani,kutokutumia pombe au vilevi vingine kama bangi au milungi.

Mkaguzi amesema jukumu lao kama askari wa usalama barabarani ni kutoa elimu bila kuchoka lakini pia kuwaonyesha madereva hao kuwa jeshi la polisi haliko barabarani kwa ajili ya kutoa adhabu tu kwa madereva wazembe bali ni pamoja na kuwaelimisha kama sehemu ya kuwakumbusha wajibu wao ni kwa vipi wanapaswa ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Zaidi ya madereva 34 wa mabasi , malori na gari ndogo kwa nyakati tofauti barabarani walipewa elimu kuhusu sheria za usalama barabarani pamoja na kupimwa kwa kifaa maalum iwapo wametumia kilevi

Zoezi hilo limeelezwa ni endelevu na madereva wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi la polisi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...