Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Ruangwa
NI upendo mkubwa kwa mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan !Ndivyo unavyoweza kuelezea namna ambavyo maelfu wananchi wa Ruangwa mkoani Lindi leo Septemba 24,2025 wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Samia Suluhu Hassan.
Katika Uwanja wa Madini uliopo Ruangwa Mjini wilayani Ruangwa mkoani Lindi umefurika huku wananchi zaidi ya 185,000 wakiwa na shangwe la kutosha kwa Mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassana huku wakipaza sauti kuwa kwa maendeleo ambayo yameyafanya ahadi yao kwake ni kumpa kura ndio na ushindi wa heshima.
Katika mkutano huo wa kampeni za kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia amekuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa alikuwa sehemu ya wana Ruangwa ambao wamempokea mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Kama unavyojua kwa CCM haina jambo dogo wanapoamua jambo leo na kwa siku ya leo wananchi wa Ruangwa walikuwa na kazi moja ya kumpokea na kumsikiliza Mgombea urais Dk.Samia lakini la kufurahisha zaidi ni namna ambavyo wananchi hao muda wote walikuwa na Vibe(shangwe).
Pamoja na yoote hayo wana Ruangwa kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamemthibitishia Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan kwamba Ruangwa na Wana Lindi wanakila sababu ya kunchagua Dk.Samia ili aendelee kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba kwa kazi aliyoifanya jukumu lao ifikapo Oktoba 29 wanakwenda KUTIKI kwake.
“Kwa mipango ambayo Rais Dk.Samia anayo kwa Wana Lindi tunamuachaje ?Kwa maendeleo ambayo ameyafanya kwetu sisi tunakwenda Kutiki kwa kumpa kura nyinyi,tunayo sababu Watanzania wenzangu tuna kila sababu ya kumchagua Dk.Samia kwa ajili ya maendeleo yetu.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...