NA MWANDISHI WETU

MANISPAA ya Ubungo imetengea bajeti ya fedha zaidi ya Sh milioni 28,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ambayo inalenga watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka minane.

Programu hiyo ilizinduliwa rasmi mwaka 2021 ambayo inatekelezwa kupitia afua tano za afya, lishe, elimu, malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama ambapo serikali inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa, watoto wenye umri tajwa wanakua katika hali ya utimilifu wake.

Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Nyamara Elisha amesema kuwa, kutengwa kwa bajeti hiyo litasaidia kuongeza chachu ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ngazi ya jamii.

Amesema kuwa, kiasi cha Sh milioni 8,960,000 zimetumika katika shughuli za afya na kiasi cha Sh milioni 9,898,000 zimetumika katika shughuli za lishe, kiasi cha milioni 4,900,000 zimetumika katika shughuli za malezi yenye mwitikio na Sh milioni 4,560,000 zimetumika katika shughuli za ulinzi na usalama wa mtoto huku elimu ya awali ikiwa haina bajeti.

Amesema kuwa, Mkoa wa Dar es Salaam una Halmashauri tano ambazo ni Kinondoni, Ilala Jiji,Temeke, Ubungo na Kigamboni ambapo kila Halmashauri inapaswa kutenga bajeti yake ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika katika utekelezaji wa Programu hiyo ngazi ya jamii, jambo ambalo litasaidia kufikisha ujumbe wa malezi.

"Ikiwa Kila Halmashauri itatenga bajeti ya fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kutoa elimu ya malezi kwa jamii, wananchi wataweza kubadilika na watoto wenye umri sifuri hadi miaka minane wataweza kukua katika hali ya utimilifu wake kwa sababu Kila mmoja ataona ana wajibu wa kumlinda na kumlea mtoto," amesema Elisha.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Bright Jamii Initiative (BJI), Irene Fugara amesema kuwa, katika utekelezaji wa Programu hiyo, serikali inashirikiana na sekta binafsi ili kuwafikia watu wengine zaidi pamoja na kutoa elimu ya malezi kwa jamii.

Amesema kwa BJI itaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha kuhusiana na malezi ya watoto Ili waweze kulwa watoto wao kupitia afua tano za malezi, jambo ambalo litasaidia kuondoa changamoto za malezi zilizopo.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...