Mgombea udiwani wa Kata ya Mabwepande kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Andrew Mashimba, leo amezindua rasmi kampeni zake kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mabwepande.

Katika mkutano huo, Mashimba alinadi sera na Ilani ya CCM, huku akieleza sababu zinazopaswa kuwashawishi wananchi wa Mabwepande kuendelea kuiamini CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.
Amesema Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameonyesha uongozi makini kwa kutatua changamoto za wananchi, hususan katika ujenzi wa madarasa, uboreshaji wa barabara na upatikanaji wa huduma za afya.

“Kwa kazi kubwa alizozifanya, hakuna kitu anachostahili Mama Samia zaidi ya kura za kishindo kutoka kwa wananchi wa Mabwepande na Tanzania kwa ujumla,” alisema Mashimba.

Aidha, ametoa wito kwa wakazi wa Mabwepande kuhakikisha wanamchagua Mbunge Geofrey Timothy, yeye mwenyewe kama Diwani, pamoja na kumpa kura nyingi za ushindi wa kishindo Rais Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe, Ndugu Geofrey Timothy, aliungana na Mashimba katika mkutano huo na kuwaomba wananchi kumpigia kura Rais Samia, Diwani Andrew Mashimba na yeye mwenyewe ili kukamilisha safu ya ushindi wa CCM.

Timothy alisema yupo tayari kushirikiana kwa karibu na wananchi wa Jimbo la Kawe kutatua kero zao mbalimbali, ikiwemo changamoto za miundombinu, ajira kwa vijana, elimu bora na upatikanaji wa huduma za kijamii.

“Nikiwa Mbunge wenu, nitahakikisha sauti ya wananchi wa Kawe inasikika bungeni. Nitapigania miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya kila mmoja wetu, kwa kushirikiana na madiwani wetu na chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Timothy.

Aliwahakikishia wananchi kuwa Ilani ya CCM 2025–2030 imelenga kuwaletea maendeleo ya haraka, na akasisitiza kuwa chama hicho kina rekodi ya utekelezaji wa ahadi zake, hivyo wananchi waendelee kukiamini.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...