Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amewataka Wanasheria kuwa walinzi na kuongeza umakini katika kutoa ushauri wa sheria zinazohusu mazingira kwa maslahi ya taifa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo tarehe 3 Septemba, 2025 wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu sekta ya mazingira yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) Jijini Dodoma.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema wanasheria hao wanatakiwa kuwa walinzi na kuongeza umakini katika kutoa ushauri wa sheria za mazingira kwa maslahi ya nchi.
“Natambua zipo changamoto wakati wa utekelezaji ,mfano uelewa mdogo wa masuala ya mazingira hivyo tunawajibu wa kuzibadili changamoto hizi na kuzifanya fursa kwa kuimarisha nafasi ya NEMC katika kusimamia sheria katika sekta ya mazingira.”Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mhe. Johari amesema mafunzo hayo yatawasaidia Mawakili hao wa Serikali kuelewa vizuri sheria na taratibu zinazohusu usimamizi wa mazingira na kufahamu majukumu ya NEMC na sheria zinazohusu ada na tuzo za kisheria.
Vilevile Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa mafunzo hayo yataongeza uelewa kwa Mawakili wa Serikali hivyo kuwasaidia wakati watakapokuwa wanatoa Ushauri wa Kisheria na Upekuzi wa Mikataba inayohusu hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.
Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini ya mifumo ya kitaasisi ili kuboresha utendaji, kwa sasa lipo andiko linalochakatwa lenye lengo la kuibadili NEMC kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Sambamba na hilo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa NEMC inatakiwa kuandaa kanuni na viwango vya ada vinavyozingatia uhalisia wa gharama za huduma pamoja na kusimamia na kudhibiti uzalishaji wa taka na uchafuzi wa mazingira na kutoza ada za udhibiti.
Awali, Mkurungenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira Tanzania (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi amesema kuwa wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kujengeana uelewa wa kisheria za usimamizi wa mazingira nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...