KATIKA kuunga juhudi za Serikali kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kampuni ya Oryx Gas Tanzania imeshirikiana na Taasisi ya Tanzania Communities Rise Foundation(TCRF) kuhakikisha shule ambazo zinawanafunzi zaidi 100 kuunganisha jiko linalotumia mfumo wa nishati safi ili kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.

Akizungumza leo Septemba 19,2025 katika hafla ya uzinduzi wa jiko linatumia mfumo wa nishati safi katika Shule ya Sekondari Yusuf Makamba iliyopo Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko na Mauzo kutoka Oryx Gas Shaban Fundi amesema kampuni yao kwa kushirikiana na TCRF  wameweka jiko la nishati safi ya kupikia kwasababu ya jitihada zao katika kuona jamii ya Watanzania inatumia nishati hiyo.

Amesema Serikali kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa na ajenda kuu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo katika taasisi zenye mikusanyiko ya watu zaidi ya 100 hivyo kufunga mfumo huo katika shule hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika eneo la nishati safi.

“Kampuni ya Oryx Gas kama wadau wa nishati safi tumeona tuoneshe mfano na kuthibitisha uwezo wetu mkubwa katika kufanya  miradi ya kufunga mifumo ya nishati safi ya kupikia.

Fundi amesema jiko la nishati safi ya Oryx katika shule hiyo unakwenda kunufaisha wanafunzi 1391 ambao wanasoma katika shule hiyo ambao kila siku wanapokuwa shule wanapikiwa chakula 

“Matumizi ya kuni na mkaa waliyokuwa wanatumia kuandaa chakula kıla siku yalikuwa makubwa lakini pia yalikuwa na changamoto za kiafya.Hapa kuna wanafunzi ,walimu na wapishi  hivyo walikuwa wanapata adha ya moshi.Hivyo Oryx kupitia maombi ya Tanzania Communities Rise Foundation kwa ajili ya kufunga majiko ya oryx katika shule hiyo pamoja na baadhi ya shule zilizopo Dar es Salaam.

Pia amesema mradi kama huo wameanza kuufunga mfumo katika shule ya sekondari Kiluvya na kufafanua wameanza kutoa udhamini kwa shule hizo mbili ambazo zote zina wanafunzi wengi  hivyo katika shule hizo matumizi ya nishati ambayo sio rafiki wa mazingira ilikuwa kubwa.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea Oryx Gas inawaita wadau mbalimbali wazungumze ili kuwawekea mifumo ya nishati safi ambayo ni mifumo bora na salama kwani inakidhi viwango vya ubora vya kitaifa na kimataifa na kubwa zaidi Oryx ina mawakala nchi nzima.

Kwa upande wake Mkurugenzi na Muanzilishi wa Taasisi ya Tanzania Communities Rise Foundation Sarah Ngoma  amesema wamechagua kushirikiana na Oryx kwasababu ndio kampuni kinara katika soko la gesi ya LPG na wanajukulana nchi kote  katika biashara ya mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake.

Pia amesema wamekuwa wakishirikiana na Oryx Gas katika matukio mengi hasa yanayohusu nishati safi sambamba na kuwezesha mamalishe kutumia nishati hiyo badala ya kutumia nishati nyingine ambazo sio rafiki wa mazingira.

“Lakini tunashirikiana na Oryx Gas kwasababu ndio inapendwa zaidi na imefika sehemu nyingi zaidi kwani ukifika vijijini mtungi ambao utuona ni mwekundu na kwa kifupi mtungi wa gesi ya Oryx unapatikqna kwa urahisi na katika maeneo yote.

“Sisi kama taasisi hatufanyi tu shughuli hizi hapa Dar es Salaam lakini tuna ratiba za nishati safi mikoani ukiwemo Mkoa wa Lindi maeneo ya vijijini hivyo kampuni ambayo inaweza kuwafikia tunaowalenga tunaona mwenye uwezo huo ni Oryx.”

Pia amesema wanayo kanzi data shule zaidi ya 10 ambazo walizifanyia utafiti lakini wameanza na shule ya Sekondari Yusuf Makamba iliyopo mkoani Dar es Salaam kwasababu iko katikati ya mji na inatumia mkaa.”Hivyo unaweza kuona wanaothirika sio tu walioko ndani ya shule bali hata wale walioko nje ya shule hii.”

Amesema kitendo cha kuona shule hiyo bado inatumia nishati chafu ndipo waliona kuwa iko haja ya kujenga mfumo wa jiko ambao utatumia nishati safi ya kupikia hivyo kwa kushirikiana na Oryx Gas wamefunga mfumo huo.

Ameongeza wameaza na shule hiyo pamoja na shule ya sekondari Kiluvya huku akitumia  fursa hiyo kuwaomba wadau ,mashirika na taasisi kusaidia zaidi kwenye taasisi mbalimbali hususani zenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili waweze kutumia Nishati safi ya gasi.

Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Yusuf Makamba iliyopo jijini Dar es Salaam Kanne Kibangali ametoa shukrani kutokana kujengewa jiko la kutumia nishati safi ya kupikia uliowekwa na Oryx Gas.

Amesema kufungwa kwa jiko la oryx katika shule hiyo kwao ni neema kubwa kwani inakwenda kurahisisha utendaji wa kazi kwasababu wanafunzi ni  ni wengi  na wanapoandaa chakula umekuwa ukitumika muda mwingi lakini kupika kwa gesi inakwenda kurahisisha kwa kuwa watatumia muda mchache kuandaa.

“Kitaaluma uwepo wa jiko la gesi ya oryx unakwenda kurahisisha sana maana sasa wanafunzi wataandaliwa chakula kwa muda mfupi watakula na kurudi darasani kuendelea na Masomo na watakuwa wanakula kwa wakati.”














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...