Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama Mhe Albert Chalamila ametembelea soko la Kawe ambalo limeungua moto usiku wa kuamkia leo Septemba 15,2025 kuwafariji wafanyabiashara waliopoteza mali zao kutokana na ajali hiyo ambapo ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kutoa kiasi cha shilingi milioni miamoja kama mkono wa pole
Akizungumza mara baada ya kutembelea soko hilo lililoteketea kwa moto kwenye eneo la kawe jijini Dar es aalaam RC Chalamila pamoja na kufikisha salam za pole kutoka kwa Rais Dkt Samia amesema soko hilo sasa litajengwa na Serikali kwa ubora na kwa haraka ili wafanyabiashara waendelee na biashara na kwamba kwa sasa wafanyabiashara wapelekwe eneo la viwanja vya shirika la nyumba NHC Tanganyika Perkas
Aidha RC Chalamila ameelekeza kuandaliwa takwimu za wafanyabiashara kwenye masoko yote ili yanapotokea majanga kuwe na takwimu sahihi za waathirika ambapo kwa soko hilo la Kawe kulikua na takribani wafanyabiashara elfu moja walioathitika hivyo ametaka Manispaa ya kinondoni kutoa milioni miamoja ya pole mapema Septemba 16, 2025.
Kwa upande wake Katibu wa wafanyabiashara wa soko la Kawe Ndg Silvester Chidego ameshukuru Serikali kwa kutoa faraja kwa wafanyabiashara na kwamba fedha hizo milioni miamoja watazigawa kwa wafanyabiashara wote huku mmoja wa wazee wafanyabiashara wa soko hilo akiomba wadau kujitokeza kuwawezesha wafanyabiashara huku akitoa tahadhari kwa vibaka walioiba bidhaa za wafanyabiashara kuwa kuna dua maalum itasomwa
Soko hilo la kawe limeungua usiku wa Septemba 15, 2025 hivyo kuamkia Septemba 16, 2025 RC Chalamila ameagiza kamati ya kuchunguza chanzo cha moto huo iwe imeundwa na ifanye kazi yake mara moja.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...