Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Jimbo la Solwa, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Edward Ngelela

Na Marco Maduhu, Shinyanga


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum, amewaomba wana CCM kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa kura zao maoni za kutafuta wagombea,ili waungane kuwa kitu kimoja na kumtafutia kura Mgombea Urais, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Amebainisha hayo leo Septemba 15,2025, wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM katika Jimbo la Solwa, kwa kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM (2025-2030) kwa wananchi, mkutano uliofanyika Kata ya Lyamidati.


Ahmed amesema, mchakato wa kura za maoni umeshapita na wagombea wameshapatikana kwa ngazi zote za Ubunge na Udiwani, hivyo ni vyema makundi yote yakavujwa na kuungana kusaka kura zikiwamo za Rais Samia ili CCM ipate kushinda kwa kishindo Oktoba 29.


"Hapa Lyamidati nasikia kuna makundi, naombeni wana CCM wenzangu tuvunjeni makundi yote yaliyokuwapo kipindi cha kura za maoni,sababu wagombea wameshapatikana tuunganeni tusake kura CCM ishinde kwa kishindo,kuendekeza makundi ni kujiumiza na kujipa presha bure,"amesema Ahmed.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa ,Ahmed Ally Salum


Aidha amekipongeza pia Chama chake pamoja na wana CCM wote,kwa kuendelea kumwamini na kumpitisha kugombea tena Ubunge katika Jimbo hilo la Solwa, kwamba hawezi kuwaangusha na wananchi atawaletea maendeleo sababu wana mfahamu vizuri kwa utendaji wake kazi.


Pia, ameshukuru kugawanywa kwa Jimbo hilo la Solwa ambalo awali lilikiwa na Kata 26, lakini sasa hivi ana Kata 12,na Jimbo jipya ya Itwangi likiwa na Kata 14, na kwamba kasi ya maendeleo itaongezeka zaidi sababu amebakiwa na Kata chache.


Aidha, akielezea wananchi maendeleo ambayo ameyafanya ndani ya miaka mitano katika Jimbo hilo la Solwa, kuwa katika sekta ya maji kati ya vijiji 68, vijiji vitano tu ndiyo vimebaki havina maji na kwamba katika bajeti ijayo endapo wananchi wakampatia ridhaa ya kuwa Mbunge tatizo hilo anakwenda kulimaliza.


Amesema kwa upande wa sekta ya Afya amejenga Zahanati nyingi na Vituo vya Afya, na kwamba katika Bajeti ijayo Kata ya Lyamidati itapewa kipaumbele kujengewa kituo cha Afya.


Ameongeza katika suala la umeme, vijiji vyote vya Solwa vina huduma hiyo, na kusalia Vitongoji vichache, na pia ameboresha miundombinu ya barabara ikiwamo ujenzi wa madaraja na makaravati.

Aidha,Ahmed ameahidi wananchi kwamba akimpatia ridhaa tena,ataendelea kuwaletea maendeleo,pamoja na kushughulia tatizo la Mgogoro wa Hifadhi.


Pia,amewahidi vijana,ataanzisha mashindano ya michezo ili kuibua vipaji vyao na hata kusajiliwa kwenye timu kubwa na kupata ajira.


"Nawaombeni sana wananchi siku ya Uchaguzi Oktoba 29 mpigieni kura za ndiyo Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan,Mimi mwenyewe na Mgombea Ubunge wa Itwangi Dada yangu Azza Hillal Hamad na Madiwani wote wa CCM ili tuendelee kuwaletea maendeleo,"amesema Ahmed.

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kampeni, amewaomba wananchi kwamba Oktoba 29 wasifanye makosa bali wamchague Rais Samia,Ahmed Ally Salum, yeye mwenyewe na madiwani wote wa CCM wala wasichanganye na wagombea wengine ili wafanye kazi kama timu moja na kuwaletea maendeleo ya kweli.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela,amewasisitiza wananchi kwamba siku ya uchaguzi Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kuchagua mafiga matatu ya CCM kwa kura za ndiyo kwa Rais Samia,Wabunge wote wa CCM na Madiwani.


Oktoba 29 ni siku ya uchaguzi mkuu wa kichagua Wabunge,Madiwani na Rais ambapo kwa sasa vyama vya siasa vipo kwenye Kampeni za kunadi sera na ilani ya vyama vyao kwa wananchi.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum na Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kulia) wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kampeni Jimbo la Solwa Septemba 15,2025 - Picha na Kadama Malunde

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum na Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kulia) wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kampeni Jimbo la Solwa Septemba 15,2025

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum akinadi sera na kuomba kura kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum akinadi sera na kuomba kura kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum akinadi sera na kuomba kura kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Ahmed Ally Salum akinadi sera na kuomba kura kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Solwa
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Edward Ngelela akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akiomba kura kwa ajili ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ahmed Salum, Madiwani wa CCM na yeye mwenyewe akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Solwa

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akiomba kura kwa ajili ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ahmed Salum, Madiwani wa CCM na yeye mwenyewe akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Solwa














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...