Vijana wameendelea kupiga hatua za kimaendeleo Mkoani Tanga Kupitia ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa waliowezeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa kushirikiana na Solidaridad.
Katika kukabiriana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana, TADB kwa kushirikiana na Solidaridad East Africa wameanzisha mpango wa kipekee unaoitwa Youth Farm Settlement (YFS), chini ya Dairy 2025 Catalyst for Investment. Mpango huu unaotekelezwa katika Mkoa wa Tanga na una lengo la kuwawezesha vijana chini ya umri wa miaka 35, kuingia kwenye sekta ya ufugaji kibiashara. Hivyo, kusudio lake si ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kwa kiwango cha kujikimu tu, bali kwa kiwango cha kibiashara kinachoweza kuwaletea kipato endelevu na kuibua ajira kwa wengine.
Katika awamu ya kwanza, vijana watano mashujaa wamepatiwa mashamba. Kila mmoja amepata shamba lenye ukubwa wa ekari 10 ambapo katika shamba hilo benki imejenga miundombinu muhimu, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kisasa kwa mnufaika, banda la ng’ombe wa maziwa la kisasa lenye uwezo wa kutunza ng’ombe kumi na ndama zao, banda la kuku wa kienyeji 200, ekari moja ya shamba la marisho ya ng’ombe, miundombinu ya maji (kisima) ya uhakika kwa ajili ya shughuli za ufugaji na umwagiliaji, pamoja na kuwapatia mitamba mitano ya ng’ombe wa kisasa wenye mimba. Lengo kuu ni kuhakikisha kila mnufaika kuwa na uhakika wa kuzalisha angalau lita 40 za maziwa kwa siku.
Matokeo ya mradi huo ni kama yafuatayo;
✅ Kila kijana anatarajiwa kuajiri angalau vijana wengine wawili, hivyo kuongeza ajira vijijini.
✅ Kila ng’ombe anazalisha wastani wa lita 8 za maziwa kwa siku, hivyo kupeleka sokoni zaidi ya lita 40 kwa kila mkulima na kuhakikisha jamii inapata maziwa ya kutosha.
✅ kuhakikisha vijana wanakuwa mfano wa kuigwa kwa wenzao na jamii iliyowazunguka wakionyesha kuwa kilimo na ufugaji vinaweza kuwa suluhisho la ajira na ustawi wa kiuchumi kwa vijana.
Kwa ushirikiano huo, TADB na Solidaridad wameweka msingi wa kizazi kipya cha wakulima na wafugaji wakibadilisha mtazamo wa vijana kuhusu kilimo kutoka “kazi ya walioshindwa” kuwa biashara yenye faida na mustakabali wa uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...