Na Pamela Mollel, Arusha


Mashindano ya Tanfoam Marathon yamezinduliwa rasmi kwa msimu wa pili, yakitarajiwa kufanyika tarehe 7 Desemba 2025 jijini Arusha katika Viwanja vya General Tire. Wananchi wa ndani na wageni kutoka mataifa mbalimbali wametakiwa kujitokeza kushiriki na kushuhudia tukio hilo kubwa la michezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mwenyekiti wa mbio hizo Glorious Temu alisema maandalizi ya mwaka huu ni ya kipekee kwa lengo la kuinua vipaji vipya vya riadha na kulitangaza Jiji la Arusha pamoja na Tanzania katika ramani ya michezo duniani.

“Michezo si burudani pekee. Ni daraja la mshikamano katika jamii, kichocheo cha afya bora na pia nguzo ya maendeleo ya kiuchumi kupitia utalii na uwekezaji,” alisema Temu.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Rogart Stephen, alisema mbio hizo zimekuwa chachu kubwa kwa maendeleo ya riadha nchini kutokana na ubora wa maandalizi na ushiriki mkubwa wa wanariadha.

Amesema kupitia mashindano ya mwaka jana, baadhi ya washiriki walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika Tokyo, Japan Septemba 13, 2025, jambo ambalo linaonyesha mchango wa Tanfoam Marathon katika kuinua viwango vya riadha kitaifa na kimataifa.

Aidha, Stephen alimpongeza mratibu na wadhamini wa mbio hizo kwa kufanikisha mashindano yenye kuvutia wadau wa michezo, na kusisitiza kuwa yataendelea kuwa chachu ya kuibua na kukuza vipaji vipya vya riadha nchini.

Mashindano haya yanatarajiwa kuvutia washiriki wa ngazi mbalimbali, kuanzia wakimbiaji wa kitaalamu, vijana chipukizi hadi washiriki wa kawaida wanaopenda michezo kwa ajili ya kujenga afya. Pia, yanatarajiwa kuleta manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa Arusha kupitia ongezeko la wageni na watalii, jambo litakaloongeza mapato kwa sekta ya biashara na huduma.

Wananchi wa Arusha na maeneo jirani pamoja na washiriki kutoka mikoa na nchi mbalimbali wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo ambazo sasa zinatajwa kama moja ya matukio makubwa ya michezo yanayoipa Tanzania hadhi ya kimataifa.








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...