Na Mwandishi Wetu,Korogwe
Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kupitia Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya hiyo Bi Edna Assey, amewaasa Viongozi wa Vyama vya siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025, kuzingatia Sheria ya Usajili wa Vyama vya siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi zinazosimamiwa na Ofisi hiyo, hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Pamoja na mambo mengine, Akitolea Ufafanuzi wa Sheria hizo wakati wa Mafunzo kwa Wenyeviti na Makatibu wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Bi Edna Aliongelea makatazo yaliyopo katika Sheria hizo na adhabu zake akitolea mfano wa matumizi ya maneno ya matusi kashfa na dhihaka yanayoweza kupelekea uvunjifu wa Amani na kuwaasa kunadi Sera za vya vyama kistaarabu kwa wafuasi na wananchi ili kuweza kuchaguliwa.
Mafunzo hayo yaliyohusisha viongozi wa vyama hivyo kutoka Halmashauri ya Mji Korogwe na Korogwe vijijini yamefanyika Tarehe 12 Septemba 20225 mjini Korogwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...