Na Pamela Mollel, Arusha

Baada ya Mji Mkongwe, Unguja kufanikisha mradi wa kufunga kamera za ulinzi (CCTV) katika mitaa yake mingi, sasa Jiji la Arusha nalo limeanza kuchukua hatua kuelekea mfumo huo wa kisasa wa usalama.

Mpango huo ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ambaye kwa sasa anawania ubunge katika jimbo la mjini hapa. Makonda aliwahi kusisitiza kuwa mbali na kuviwezesha vyombo vya ulinzi kwa vifaa na nyenzo, jiji linahitaji kuwa na kamera za CCTV ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao.

Lengo kuu la mpango huo ni kuwapa wafanyabiashara uhakika wa kuendesha shughuli zao hadi usiku bila hofu ya uporaji, hivyo kuongeza mzunguko wa uchumi wa jiji.


Wananchi wahimizwa kufunga pia majumbani na kwenye biashara

Pamoja na mradi wa serikali kufunga kamera katikati ya jiji, wakazi wa Arusha wameshauriwa pia kuwekeza katika kamera za ulinzi majumbani mwao na kwenye biashara binafsi, ili kuongeza uimara wa usalama.

Lakini swali kubwa ni: je, mradi huu una gharama kubwa na unaweza kufikiwa na kila mtu?

Wataalamu wa CCTV watoa majibu

Mmoja wa wataalamu wa mifumo ya usalama, Saidi Mringo kutoka kampuni ya Sagrass Digital Technologies, anawaondoa hofu wakazi wa Arusha akisisitiza kuwa kamera za CCTV si ghali kama wengi wanavyodhani.

“Faida zake ni kubwa mno. Mtu anaweza kuona chochote kinachoendelea nyumbani au kazini hata akiwa safarini,” alisema Mringo.

Anabainisha kuwa teknolojia hiyo si ya miji pekee bali hata vijijini—hasa kwa wakulima na wafugaji.

“Kwa mfano, mkulima mwenye boma kubwa la mifugo akifunga kamera, hakuna maziwa yatakayokamuliwa na kuibiwa bila yeye kujua,” alifafanua.

Kwa mujibu wa Mringo, dunia inasogea katika mwelekeo ambao kila mtu atahitaji kutumia CCTV kwa ajili ya kujilinda na kulinda mali zake.

Gharama na upatikanaji

Mtalaamu huyo anasema mteja anaweza kuanza na kamera moja au mbili kulingana na uwezo, kisha kuongeza taratibu.

“Kuhusu umeme kukatika, kamera nyingi tunazofunga huwa na backup hivyo zinaendelea kufanya kazi bila tatizo,” alisema.

Usalama wa kamera zenyewe

Kuhusu uwezekano wa kamera kuibwa au kuharibiwa, Mringo anabainisha kuwa mafundi hufunga vifaa hivyo sehemu za juu zisizofikika kirahisi na kuzipa kinga imara mithili ya sanduku la pesa.

Kampuni yake inajihusisha zaidi na kamera aina ya Analogue na IP, ambazo zina uwezo wa kufanya kazi saa 24 na kurekodi picha zenye ubora wa juu hadi umbali wa kilomita moja.

Wito kwa wananchi

Mringo anatoa wito kwa wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kuanza kutumia kamera za CCTV ili kuendana na teknolojia ya sasa na kujihakikishia usalama wa mali zao.

Saidi Mringo (maarufu pia kama Saidi Macable) hupatikana Arusha, mkabala na Shule ya Sekondari Bondeni, ambapo anaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya kutumia kamera za usalama.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...