CHAMA Cha Magari wamesema Wataendelea na Harakati za Kuhakikisha Madereva Wanafata Sheria za barabarani na kwa kutoa elimu za Usalama na Kuandaa Mashindano mbalimbali ya michezo ya magari.
Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi wa Chama cha Magari nchini Najma Rashid wakati wa ufunguzi wa Shindano la Magari Kwa Vijana lililofanyika Masaki Jijini Dar es Salaam amesema Shindano hilo lina lengo na dhamira ya Kuhakikisha Harakati za Usalama na Sheria za barabarani kwa Madereva zinaendelea Kufatwa kwa mashindano hayo ya Magari.
Nae Kwa Upande Wake Mshiriki wa Shindano hilo amesema Kama Kijana inamjengea uthubutu na kujiamini hasa anapokuwa katika Mashindano hayo
"Shindano hili linalenga kupima mchujo wa awali kwa Dereva chipukizi kujua uwezo wake namna ya Kuendesha gari kwa Usalama na Kutunza chombo chake hivyo pia kwa Vijana ni fursa kubwa kwani inatupa nafasi ya kushiriki shindano la Kimataifa nchini Kenya."
Pia Mwalimu wa Udereva Kutoka Chama cha Magari nchini (AAT) Juma Rashid ameongeza kuwa Shindano linasaidia zaidi Kupata Vijana Mahiri wenye weledi na uwezi wa Kutunza vyombo vyao kwa muda mrefu kutokana na uendeshaji wao kwa sababu wanafata sheria zote na kuhakikisha usalama wao pamoja na chombo..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...